Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2024








🔴Apokelewa na Katibu Mkuu na Wafanyakazi wa Wizara

🔴Aahidi kushirikiana na wadau kumsaidia Mhe. Rais kufikia malengo

Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio  amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma, alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha. Felchesmi Mramba, menejimenti na watumishi wengine wa Wizara ya Nishati.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dkt. Mataragio amesema ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi wa kitaifa na Taifa kwa ujumla.

 "Mimi  nashukuru kuteuliwa kutumikia nafasi hii, nitaendelea kushirikiana na watumishi wenzangu ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake." Amesema Dkt. Mataragio.
Posted by MROKI On Monday, March 11, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo