Mkurugenzi wa Uchunguzi wa
Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho
Mtega (katikati) akikabidhi vifaa Kinga vya maabara kwa Kaimu Afisa Elimu
Sekondari wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (kulia) baada ya kutoa mafunzo ya
usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa shule ya Sekondari Kitomondo katika
Wilaya ya Mafia Februari 1, 2024
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo, Ayen Mathias,
akiuliza swali kwa wawezeshaji katika mafunzo ya Usimamizi na udhibiti wa
kemikali za viwandani na majumbani yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali shuleni hapo.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Kitomondo wakifuatilia mafunzo ya usimamizi na udhibiti
wa kemikali za viwandani na majumbani kutoka kwa wawezeshaji kutoka Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (hawapo pichani).
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki, Stanford Mwasilonda,
akiwasilisha mada kuhusu madhara ya Kemikali kwa washiriki wa mafunzo ya
matumizi salama ya kemikali.
Mtumishi wa Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Elice Omary (aliyesimama)
akiwasilisha mada kuhusiana na alama mbalimbali za tahadhari za kemikali.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (kushoto) akiongea
na walimu wa shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kutembelea maabara ya Shule hiyo
iliyopo wilayani Mafia.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitomondo wilayani Mafia, Ramadhani
Janabi (aliyesimama) akiwakaribisha timu ya wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika
Mafunzo ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani kwa
walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo yaliyofanyika katika shule
hiyo Februari 01 2024.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa
pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka
(aliyekaa kulia), na Walimu wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya
kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa
pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka
(aliyekaa kulia), na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya
kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara katika shule
hiyo.
***************
Na Mwanaheri Jazza
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali Imetoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti salama wa kemikali
pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya kazi za Maabara kwa
wanafunzi na walimu wa sayansi katika shule ya Sekondari Kitomondo wilayani
Mafia Mkoa wa Pwani.
Akizungumza wakati wa ugawaji
wa vifaa hivyo, Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,
Kanda ya Mashariki, Elice Omary, amesema utoaji wa vifaa hivyo utasaidia
kuwakinga wanafunzi hao na athari mbalimbali zinazoweza kijitokeza wakati
wakifanya mafunzo Kwa vitendo wawapo maabara.
"Tumepata fursa ya kuwapa
elimu walimu na wanafunzi wa shule hii ya Kitomondo juu ya madhara
yanayopatikana na matumizi mabaya ya kemikali na jinsi ambavyo wanaweza
kujikinga, pia tumetoa baadhi ya vifaa Kinga Ili watakapokuwa wakifanya mafunzo
kwa vitendo waweze kujikinga na athari mbalimbali zinazotokana na matumizi
yasiyo sahihi ya kemikali" alisema Elice.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kitomondo Ramadhan Janabi amesema vifaa Kinga hivyo
vitasaidia walimu na wanafunzi kujikinga wakiwa katika mafunzo ya vitendo Kwa
kuwa Maabara Kuna kemikali Hatarishi.
"Kwetu sisi huu msaada
utasaidia sana Kwa kuwa tunafahamu maabara Kuna kemikali ambazo ni hatari kwa
mwili wa binadamu, hivyo wanafunzi na walimu wanaofundisha watavaa na kuwa
salama" alisema Mwalimu Mohamed.
Nao baadhi ya wanafunzi wa
shule hiyo, Amina Athumani na Ayen Mathias wameishukuru Mamlaka kwa kuwapatia
vifaa vya kujikinga wakati wakifanya mafunzo kwa vitendo".
"Tunaishukuru Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutuletea vifaa hivi kwani ni msaada
mkubwa kwetu tutajikinga na kemikali hatarishi tukiwa maabara" walisema
wanafunzi hao.
0 comments:
Post a Comment