Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa Kanda ya Dar es Salaam kuanzia Januari 24 -30, 2024 na yatahitimishwa Februari Mosi Siku ya Sheria Duniani.
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inashiriki maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali juu ya Majukumu ya Mamlaka na kama mdau muhimu katika mnyororo wa Haki Jinai.
Maadhimisho hayo yanabebwa na kauli mbiu “ Umuhimu Wa Dhana Ya Haki Kwa Ustawi wa Taifa, Nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mifumo Jumuishi ya Haki Jinai”
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. David Ngunyale (kushoto) akipata maelezo juu ya majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka katika uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za makosa ya jinai kutoka kwa mtumishi wa Mamlaka Muhsin Kilonzo (kulia) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Wananchi mbalimbali watembelea banda la Mamlaka kupata elimu juu ya Majukumu ya Mamlaka kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Wananchi mbalimbali watembelea banda la Mamlaka na kusaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (kushoto) akitoa elimu juu ya majukumu mbalimbali ya Mamlaka kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Mhe. Abdallah Hassan Gonzi, (kushoto) akitoa ushauri baada ya kupata maelezo juu ya majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka kutoka kwa mtumishi wa Mamlaka, Muhsin Kilonzo (kulia) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Wananchi mbalimbali watembelea banda la Mamlaka na kusaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (kushoto) akitoa elimu juu ya majukumu mbalimbali ya Mamlaka kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment