Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuozesha watoto wao wa kike huku akiwasisitiza kutoa kipaumbele kwenye kuwahimiza kusoma na kudumisha maadili mema katika jamii.
Ameyasema hayo leo Novemba 23 katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi kukagua miradi inayotekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya kiongozi wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Akiwa katika Kijiji cha Handa Kata ya Handa Wilaya ya Chemba, amesema wazazi wamejisahau hususan katika suala la malezi hali inayopelekea mmomonyoko wa maadili kwa watoto.
“Tunataka watoto wetu wasome vizuri na wafaulu vizuri kwani ndio lengo la Serikali na ndio maana kuna ongezeko kubwa la shule katika jamii zetu ili kudumisha Elimu katika kila kijiji na kata"
"Wazazi acheni tabia ya kuozesha watoto na kuwafanya wakatishe masomo yao, kila mtoto ana ndoto ya kufika Mbali na si kuwaozesha, acheni watoto wasome na ndio maana kila Wilaya kuna Chuo cha Veta ili watoto waweze kujiendeleza kiufundi zaidi” amesisitiza Chatanda.
Aidha miradi iliyokaguliwa na kiongozi huyo ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Chemba iliyopokea kiasi cha Shilingi 3,214,000,000, Mradi wa Mabweni ya shule ya Msakwalo iliyopokea kiasi cha shilingi 707,8000,000, na Mradi wa Shule ya Handa iliyopokea kiasi cha Shilingi 588,400,000.

Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Mary Chatanda Novemba 23,2023 umeendelea na ziara yake ikiwa ni siku ya pili umefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani humo.
Uongozi huwa ukiwa katika ziara yake umegawanyika katika timu mbalimbali ambapo Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande amefanikiwa kutembelea mradi wa Ujenzi wa Vyumba 4 vya madarasa na Ofisi 3 katika Shule ya Msingi Mwaikisabe wenye thamani ya Shilingi 90,000,000 (Millioni tisini) kituo cha Afya zahanati ya Soya iliyopo kata ya Soya pamoja na kusikiliza kero za wananchi .
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Soya na Kimaha amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda walinzi kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .
"Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao ambayo bado wanayo kubwa ,hatuwezi kukaa kimya hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao na miili yao utasikia huko mara mtoto amelaitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande
Vilevile, Ndg .Kingwande amefanikiwa kusikiliza kero za wananchi hao na kuzipatia ikiwemo ahadi ya muda mrefu ya gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati ya Soya na zingine ameielekeza Halmashauri ya Chemba kuwafanikishia wananchi wake likiwemo suala la TASSAF ,Barabara, ujenzi wa shule Vyumba vya madarasa 4 katika Shule ya Chang'ombe na Kata hio,pamoja mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi .










0 comments:
Post a Comment