Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2023









Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo mradi wa Bwawa la Membe na mradi wa Skimu ya umwagiliaji Chinangali chini ya Mradi wa Building Better Tomorrow (BBT) katika Wilaya ya Chamwino. 

Akizungumza Leo Novemba 11,2023 Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Omary Kigua wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyoanzia Mkoa wa Dodoma na inatarajia kufanyika kwa siku saba katika Mikoa mingine tofauti tofauti ikiwemo Manyara, Arusha, Singida, Tabora ,Iringa na kukamilika katika Mkoa wa Mbeya.

Amesema ziara hiyo ina lengo la kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo. 

“Tumeridhika na shughuli zinazoendelea hapa na kiasi cha fedha ambacho kimetumika hakika kinasadifu kwamba kazi mnaisimamia vizuri ". Ameeleza Mhe. Kigua

Aidha, amewahimiza  wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali popote utakapo hitajika kwani kukamilka kwa mradi huo itakuwa chachu kwa wananchi wote ambao wapo jirani na maeneo hayo ya miradi kwa  kuwa wao ndio wanufaikaji  wa kwanza na ndiyo dhamira ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kuinua maisha ya wananchi wa chini. 

Kwa Upande Wake, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametumia fursa hiyo kuelezea azma ya Serikali katika kuhakikisha wanamuwezesha mkulima kuzalisha kipindi chote cha mwaka  bila kutegemea mvua.

“ Lengo letu kama Wizara tunataka Wananchi waweze kufanya shughuli za Kilimo mara mbili hadi tatu kwa mwaka wasitegemee mvua , Pia  mradi huu  hautakua kwa ajili ya kilimo tu bali hata wafugaji  watatengenezewa banio kwa ajili ya kunyweshea ng'ombe na shughuli za uvuvi pia zitafanyika.” Amesema Silinde

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Mhe. Rais kwa kufanya Mapinduzi ya Kilimo ndani ya Mkoa huo ambayo yatasaidia kuondoa njaa ,udumavu na kitakuwa chanzo cha uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

Ameahidi kuendelea kuwa karibu na wakandarasi ili fedha zilizotolewa na Serikali ziweze kufanyiwa kazi husika na kwa ufanisi .
Posted by MROKI On Saturday, November 11, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo