Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2023




Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameyasema utatuzi wa kero katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Chalinze utatatuliwa na wananchi wenyewe. 


Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Halmashauri Wilayani hapo. 

Akizungumza katika mkutano huo , Ndg. Kikwete amewakumbusha madiwani kuwa mbele katika kutatua kero za wananchi na sio kusubiri viongozi wanaowaita “wa juu” ili waje kutatua kero katika maeneo yao. 

Mbunge aliwaasa wajumbe kushughulikia kero za wananchi katika maeneo yao pale zinapotokea bilq kupoteza muda. 

Katika mkutano huo pia, Ndg. Mawazo Mkufya alichaguliwa kwa kura 19 kati ya 21 zilizopigwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika kipindi cha Mwaka mmoja na kamati za madiwani pia ziliundwa upya na kupata viongozi pia.

Posted by MROKI On Sunday, September 03, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo