Nafasi Ya Matangazo

August 09, 2023

Ziara Mhe. Prof Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji leo tarehe 9 Agosti, 2023 amefanya ziara ya kikazi mkoani Pwani na kutembelea wawekezaji wa Sapphire Float Glass watakao husika na utengenezaji wa vioo na uzalishaji unatarijiwa kuanza mwezi Septemba, 2023. Uwekezaji huu unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 1650. Aidha, Waziri Mkumbo amesisitiza nia ya serikali kuendelea kujenga mazingira bora na rahisi ya uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji zaidi wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujitosheleza kwa bidhaa na kuongeza thamani ya didhaa zinazosafirishwa nje ya nchi na kujipatia fedha zaidi za kigeni.

Posted by MROKI On Wednesday, August 09, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo