Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi hususani vijana
kutumia fursa ya uwekezaji katika kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo
tarehe 4 Agosti, 2023 wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wakulima na
Wafugaji (Nane-Nane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini
Mbeya.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa
kila Mwananchi kuungana na Serikali katika kutimiza azma ya kufanikisha
mapinduzi ya kilimo nchini yanazaa matokeo chanya.
"Serikali yetu
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuwekeza na
kuwawezesha vijana kujikita katika kilimo ikiwemo uanzishwaji wa mradi wa
mashamba makubwa ya kuwezesha vijana kulima kibiashara (BBT) hivyo basi hakuna
budi kila mmoja kuona ipo tija ya kushiriki katika uwekezaji huu"
Amesisitiza Dkt. Tulia
0 comments:
Post a Comment