Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2023



Tume ya Madini imeibuka Mshindi  wa Pili kwenye Kundi la Watoa Huduma wa Taasisi za Serikali  na kupewa Tuzo ya Utoaji wa Huduma Bora kwenye Maonesho ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Katika hatua nyingine Tume ya Madini  imekuwa mshindi wa pili na kupata tuzo ya kombe pamoja na cheti kutoka Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kwa kutambua mchango  wake mkubwa katika  maonyesho hayo.

Akizungumza mara baada ya Tume kunyakua tuzo hizo, Msimamizi wa Banda la Tume, Adrian Anthony amesema kuwa siri ya kupata tuzo hizo ni pamoja na kutoa huduma bora kwa watembeleaji wa maonesho ikiwa ni pamoja na kuonesha fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini, namna ya kutambua madini mbalimbali na kutatua changamoto zilizokuwa zinawasilishwa na wadau waliotembelea maonesho hayo.
Posted by MROKI On Wednesday, August 30, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo