Nafasi Ya Matangazo

August 22, 2023

 
Kocha wa timu ya Taifa, Denis Lungu(kulia) akizungumza na baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Pooltable (baadhi wapo pichani na baadhi hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi cha kukaribisha wachezaji wa timu ya taifa walioteuliwa kuripoti kambini kwa mchujo maalum wa kupata kikosi bora cha kuwakilisha Nchi kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Octoba Nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Pool Taifa na Wachezaji walioteuliwa kuripoti kambi ya timu ya Taifa   wakiwa katika kikao kifupi cha kuwekana sawa kabla ya kuanza mazoezi rasmi ya mchujo wa kupata timu ya Taifa cha kuwakilisha Nchi kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Octoba Nchini Afrika Kusini.
*********
Na Mwandishi wetu.
KIKOSI cha timu ya Taifa cha mchezo wa Pooltable leo kimeanza rasmi kambi baada ya tangazo  la kutajwa  sambamba na kuitwa kambini wachezaji 17 watakaoingia katika mchujo wa kupata kikosi kitakachowakilisha Nchi kwenye mashindano ya Afrika(AAPA) yanayotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu Nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na wachezaji wakati wa kikao kifupi cha kukalibisha Wachezaji Kambini, Meneja wa timu ya Taifa, Patrick Nyangusi alisema anategemea kuona mambo mapya na mazuri katika kambii hii kwa mjuano wa kupata nani sahihi wa kuwakilisha nchi, naomba kila mtu ajitume kwa kadri ya uwezo wake ili mpaka tupate changamoto za kuchagua nani aende Afrika Kusini na nani abaki.

Nae Kocha wa timu ya Taifa, Denis Lungu aliwakaribisha kambini Wachezaji  na kuwaambia wazi kuwa uwezo wako ndio utakupeleka Afrika kusini au kubaki Tanzania na kutuangalia mitandaoni.

Alisisitiza Lungu, sitambeba mchezaji bali mchezaji ajibebe kwa uwezo wake kuanzia leo katika kambi hii.Muda tulionao ni mchache sana lakini kwasababu kambi hii si ya kufundisha mchezaji kucheza naamini haitakuwa ngumu.

Lungu alimaliza kwa kuwakaribisha wachezaji wote kambini waliopata bahati ya kuteuliwa na kuwatahadhalisha kuwa wasijione kuwa bora kuliko walioachwa bali wao wameonekana wanaweza kuwakilisha Nchi wa vigezo vilivyoangaliwa na Viongozi wa chama cha Pool Taifa(TAPA).

Afisa habari wa Chama cha Pool Taifa, Lilian  aliwataja wachezaji walioripoti kuwa ni Seif Hamadi, Festo Yohana, Issaya Paul, Abdallah Hussein, Mussa Mkwega, Innocent Sammy, Melkizedeck Amadeus, Norbeth Kobelo, Jackson Steven, Charles Venance, Anthon Thomas, Said Jumanne, Abdallah Miraji, Aboubakar Salum na Abdul Said Kiande .

Wachezaji ambao mpaka sasa hawajaripoti ni Baraka Jackson kutoka Manyara na Yasin Athuman kutoka Dodoma ambao wataripoti kesho Kambini.

Lilian  alisema kuwa kambi itakuwa katika klabu ya Snipers Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaam na kama kutakuwa na mabadiliko yoyote watatoa taarifa.Muda wa mazoezi  yatakuwa yanaanza saa kumi jioni na kuendelea.
Posted by MROKI On Tuesday, August 22, 2023 1 comment

1 comment:

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo