Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2023

NAIBU  Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel  akizungumza.
Na Patricia Kimelemeta
NAIBU  Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema kuwa msongo wa mawazo Kwa mjamzito ni miongoni mwa sababu zinazoathiri afya ya Mtoto akiwa tumboni.

Akizungunzia Mkoani Dar Es Salaam katika uzinduzi wa wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 8, ambapo Dk. Mollel amesema kuwa wajawazito wanatakiwa kukaa katika mazingira yasiyowaletea msongo wa mawazo katika kipindi chote cha ujauzito na hata wanapojifungua na kuyonyesha ili kufanya maziwa yatoke vizuri na mtoto kupata lishe bora na kukua vizuri.

Amesema kuwa  mjamzito anahitaji matunzo  na kula vyakula vyenye virutubisho kwa. ajili ya lishe bora ya mtoto tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili Kwa sababu ndiyo kwenye msingi bora wa ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.

Dk. Mollel alisema, kuwa idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee  imeongezeka kutoka 58% mwaka 2018 hadi kufikia 64% mwaka 2022.

"Takwimu ya watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa imeongezeka kutoka 53.5% mwaka 2018 hadi kufikia 70% mwaka 2022.

“Siku 1000 za mwanzo, mtoto anahitaji lishe bora ambayo itajenga afya ya mtoto  ili aweze kukua kimwili na kiakili,  hii inatokana na mama anayenyonyesha kupata lishe bora ambayo itajenga kiafya na kumuondolea msongo wa mawazo," amesema Dk. Mollel.

Ameongeza  kuwa, hayo ni mafanikio makubwa ambapo Serikali itaendelea kuahirikiana na wadau mbalimbali Ili kutoa elimu kwa wananchi kuona umuhimu wa kumnyonyesha watoto.

Amesema kuwa ikiwa hatakosa lishe bora linaweza kumsababishia msongo wa mawazo ambapo mtoto hatakosa  lishe bora na kumsababishia  kupata madhara mbalimbali ikiwamo  udumavu wa mwili na akili.

Amesema  kuwa, hivyo ni muhimu mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita ya mwanzo na hapo anaweza kuendelea kunyonyeshwa huku akipatiwa chakula cha nyongeza hadi anapotimiza miaka miwili au zaidi.

Amesema kuwa watoto wadogo na watu wazima wanapaswa kula lishe bora ili kuimalisha afya zao na kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na kutokula lishe isiyokamilika.

“Kuna magonjwa mengi yanayotokana na kutokula lishe kamili ni vyema watoto na watu wazima kuzingatia hilo, pia lishe inayozidi inasababisha uzito uliozidi na hivyo kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Figo na moyo.” amesema.

Naye Mwakilishi wa wadau wa Lishe nchini kutoka UNICEF Bw. Patrick Codjia ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya dhati ya kuboresha lishe, afya na maisha ya wananchi wake ikiwa ni pamoja na watoto.

" UNICEF itaendelea kuahirikiana na serikali ya Tanzania Ili kuboresha afya ya watoto Ili waweze kupata lishe bora na kuwaondoa kwenye madhara ya udumavu," amesema Codjia.

Kwa upande wake,  Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Bi. Chiku Semfuko ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa muda kwa wanawake kwenda kunyonyesha pia kutenga vyumba maalumu vya kunyonyesha ili kuwapa nafasi wanaonyonyesha.
Posted by MROKI On Thursday, August 03, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo