Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mambamba Tandahimba kabla ya kumpatia fursa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
*************
Na James Mwanamyoto (OR-TAMISEMI)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 331 kupitia mradi wa BOOST
zilizojenga madarasa yatakayotatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika
shule ya Msingi ya Mambamba ‘B’ Wilayani Tandahimba.
Mhe. Ndejembi amesema hayo akiwa
katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, mara baada ya Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kumpatia fursa ya
kuzungumza na wakazi wa eneo hilo.
Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, Rais wa
Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitafuta zaidi ya bilioni 230 kwa
ajili ya kujenga shule mpya na madarasa nchi nzima kupitia Mradi wa BOOST kwenye
maeneo ambayo shule zina msongamano wa wanafunzi au hakuna shule, ambapo
Tandahimba imenufaika na ujenzi wa shule ya Msingi ya Mambamba ‘B’ iliyogharimu
milioni 331.
“Mhe. Waziri Mkuu milioni 331
imejenga madarasa haya mazuri yenye kupendeza katika Shule hii ya Msingi ya
Mambamba ‘B’ ambayo yatasaidia kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi uliopo
katika shule mama ya Mambamba, ikiwa ni pamoja na kuwaondolea hadha wanafunzi kutembea
umbali mrefu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Halmashauri ya Wilaya
ya Tandahimba imepokea milioni 95 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wa
shule ya msingi na milioni 95 nyingine kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu
wa shule za sekondari.
Aidha, Mhe. Ndejembi amesema TARURA
imetenga fedha kwa ajili ya kukarabati barabara ya Kilomita 7.2 ya kutoka
Mambamba kwenda Mwimbi hadi Tandahimba ili iweze kupitika katika majira yote.
Wananchi wakionesha bango la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu ya elimu Wilayani Tandahimba kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP.
Mwonekano wa madarasa ya Shule ya Msingi Mambamba ‘B’ yaliyojengwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akielekea kukagua miundombinu ya elimu inayojengwa na Serikali katika Shule ya Msingi Mambamba ‘B’ kupitia mradi wa BOOST.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi kabla ya kuzungumza na wananchi wa Mambamba Wilayani Tandahimba.
Wananchi wa Tandahimba wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipopewa fursa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kuzungumza nao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Mambamba Tandahimba alipopatiwa fursa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kuzungumza na wananchi hao.




0 comments:
Post a Comment