Mwanamuziki Mkongwe na mwanasiasa wa Tanzania aliyepata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro, Joseph Haule maarufu Prof. Jay amejitomeza dhaharanu kupitia account yake ya Social Media ya Instagram @professorjaytz na kuandika Salam za shukrani alizoambatanisha na picha yake akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wa Serikali na chama cha Mapinduzi kwa msaada mkubwa wa matibabu ya ndani na nje ya nchi.
Prof Jay pia alimshuruku Mwenyekiti wa Chama chake cha CHADEMA na viongozi pamoja na Watanzania kwa msaada wao mkubwa wa kuhakikisha anapata matibabu Bora kwa kushirikiana na Serikali.
Huu hapa ujumbe wake:
"#Repost @professorjaytz @download.ins
---
Salaam Ndugu zangu,
Kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, Asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).
Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi ,Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.
Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda @freemanmbowe ,Wanachama na viongozi wote waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali, Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu ,AHSANTENI SANA.
Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.
Shukrani sana kwa @malisa_gj na @iamlyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama @Cloudsfmtz @Millardayo @wasafifm na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea MUNGU awabariki sana kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea MUNGU AWABARIKI SANA.
Nitakuwa mchoyo wa Fadhila nisipoishukuru Familia yangu Mke wangu ( @Mke_wa_profjize ), kaka zangu, dada zangu Wadogo zangu na Familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mliomipa.
Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻
Ahsanteni
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon ❤️❤️❤️❤️"
Mwisho wa kunukuu Salam za Prof. Jay.





0 comments:
Post a Comment