Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Washereheshaji kupitia Chama Chao Cha Kisima cha Mafanikio (KCM) leo Aprili 4, 2023 jijini Dodoma wakati afungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai Kwa wadau wa Sekta za wizara yake kuzungumzia na kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kutumia taaluma na vipaji walivyonavyo.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai hiyo leo Aprili 4, 2023 jijini Dodoma alipofungua  Mkutano Mkuu wa  Chama Cha Washereheshaji  cha Kisima cha Mafanikio (KCM) ambapo amesema wadau hao wana nafasi kubwa katika kuzungumza na kuisaidia jamii kuepuka masuala yanayokiuka maadili mema yakiwemo ya unyanyasaji, ukatili na mila ambazo sio za Kitanzania.

"Natoa Rai kwenu Waneni (MC's) muendelee kuunga mkono juhudi za Serikali na mafanikio yake kwa kuendelea kutumia fursa zilizopo ikiwemo kupata mikopo nafuu kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa lakini pia kuwa mabalozi Wazuri wa Matumizi sahihi na sanifu ya Lugha ya Kiswahili" amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.

Awali muanzilishi wa Chama hicho Bw. Brison Makene amesema mkutano huo una lengo la kukumbushana namna ya kuboresha kazi zao, kuzirasimisha pamoja na kubadilishana uzoefu.

Mkutano huo umewakutanisha Washereheshaji, Wahamishaji, Watunzi wa Fasihi na  Wapambaji kutoka Kanda za  Tanzania ikiwemo Kanda ya Kati, Magharibi, Mashariki na Kaskazini.



Posted by MROKI On Tuesday, April 04, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo