Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametumia sehemu ya hotuba yake akihitimisha ziara yake nchini Afrika ya Kusini kusifu mafanikio ya filamu aliyoshiriki kunadi utalii, biashara na uwekezaji nchini Tanzania ya “Tanzania; The Royal Tour” kuwa imeleta watalii wengi zaidi katika Taifa hilo la Afrika Mashariki lenye vivutio lukuki.
Akizungumza wakati wa kikao
chake na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, wafanyabiashara na
watendaji kutoka nchi hizo mbili, Rais Samia, amewaalika wawekezaji kuwekeza
nchini Tanzania katika sekta mbalimbali huku akisisitiza kuwa sekta ya utalii
inahitaji hoteli nyingi zaidi hivyo wachangamkie fursa hiyo.
Mkutano huo wa Pili wa Tume ya
Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika
Kusini umehitimishwa leo Machi 16, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Afrika ya Kusini (CSIR ICC).
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mawaziri, Makatibu wakuu na viongozi wengine mbalimbali wa serikali
0 comments:
Post a Comment