Nafasi Ya Matangazo

March 04, 2023

 NA K-VIS BLOG
Mbunge wa jimbo la Mbagala, jijini Dar es Salaam, Mhe. Abdallah Chaurembo ameahidi kutoa TZS Milioni 2 kukamilisha ujenzi wa Kituo Kidogo Cha Polisi (Police Post), Kata ya Mbagala-Kiburugwa.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Njau, Kata ya Kiburugwa Machi 4, 2023.

Alisema Kituo hicho kimejengwa kutokana na michango ya wananchi, Mbunge na Diwani wa Kata hiyo.

“Nadhani mmeona maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa Kituo chetu Cha Polisi, kazi iliyobaki ni kupaua, mimi kama Mbunge wenu nitatoa shilingi Milioni 2,000,000/= ili tukamilishe ujenzi kwa kuezeka.”Alisema.

Kuhusu msongamano wa wanafunzi, Mhe. Chaurembo amesema Shule ya Msingi Kingugi yamejengwa madarasa mawili (2) na Shule ya Msingi Kiburugwa yamejengwa madarasa mapya 2 na vyoo 18 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 59.8.

Kiburugwa yamejengwa madarasa 2 yenye thamani a shilingi Milioni 40,

Jumla ya Fedha zilizotumila kuboresha zaidi ya shilingi Milioni 100.

Aidha alisema mgogoro uliokuwepo wa nyumba za makazi zilizokuwa ndani ya eneo la shule ya Sekondari Kingugi umetatuliwa kwa wamiliki wake kulipwa fidia na nyumba hizo  kubomolewa na kujengwa madarasa 4.

“Madarasa hayo yamekamilika na wanafunzi wanaingia madarsani.” Alifafanua.

Kuhusu miundombinu ya barabara, alisema kwa muda mrefu imekuwa ndio kilio kikubwa cha wananchi wa Kata ya Mbagala Kiburugwa.

“niliwaahidi moja ya kipaumbele changu ni barabara ya kutoka Kona Bar, Magenge 20, tayari awamu ya kwanza imeanza ya ujenzi, na sasa tunaanza awamu ya pili na bilashaka mmeona wakandarasi wako kazini.” Alisema na kuongeza..

“ Jumla ya shilingi Milioni 391  zimetumika kuboresha barabara za Kiburugwa kwa kiwango Cha Zege”. Alifafanua Mhe. Chaurembo




Posted by MROKI On Saturday, March 04, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo