Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru amefariki dunia leo Jumamosi Novemba 9, 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameomboleza kifo cha mafuru na kutoa pole kwa familia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji).
“salamu za rambirambi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Profesa Kitila Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo Novemba 09, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India," amesema Samia katika salamu zake za rambirambi.
Rais Samia amesema Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
"Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu mahali pema,"
Mafuru aliyekuwa mtaalamu wafedha na uchumi maarufu hapan chini, amehudumu katika taasisikubwa tofauti kwa miongo miwili.
Amewahi kuwa Msajili wa Hazina na Ofisa Mtendaji mkuu wa Benki ya NBC Tanzania.
Pia amewahi kuwa Naibu Katibu wa Wizara ya Fedha, Mwenyekiti waC hama cha Mabenki nchini (TBA) nam wanzilishi wa mwenza wa kampuniya ushauri wa masuala ya fedha ya Bankable.
0 comments:
Post a Comment