Nafasi Ya Matangazo

March 04, 2023

TANESCO yakabidhi kisima cha maji Shule ya Msingi Nyani, Wilayani Kisarawe 
Mkurugenzi wa fedha TANESCO CPA Renata Ndege akimtua ndoo ya maji mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyani Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa fedha TANESCO CPA Renata Ndege aipongeza Shule ya Msingi Nyani kwa kuongeza ufaulu na nidhamu shuleni.
Mkurugenzi wa fedha TANESCO CPA Renata Ndege akikabidhi vifaa vya masomo kwa mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Nyani.
Mkurugenzi wa fedha TANESCO CPA Renata Ndege akipanda mti Shule ya Msingi Nyani Wilayani Kisarawe.
*********
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limendelea na jitihada zake za uwajibikaji kwa jamii kwa kusadia uchimbaji wa Kisima Shule ya Msingi Nyani iliyoko Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Akizungumza Mkurungezi wa Fedha TANESCO Bi. Renata Ndege kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Maharage Chande amesema licha ya shughuli ya TANESCO kuwa ni huduma ya umeme, lakini wajibu wa kuisaidia jamii inayoihudumia limekuwa jambo la muhimu kwa Shirika.

“Tumekuja kukabidhi kisima cha maji chenye thamani ya shilingi milioni 14, ambacho kitawasadia wanafunzi na wanakijiji wa Nyani kuondokana na changamoto ya upatikanaji maji safi waliyokuwa wanakumbana nayo awali” alisema Bi. Ndege.

Aliongeza kuwa sambamba na kukabidhi kisima hicho wametekeleza zoezi la upandaji wa miti 100 katika eneo la Shule ya Msingi Nyani, ikiwa ni muendelezo wa mikakati ya Shirika katika kutunza mazingira.

“Sote tunafahamu umuhimu wa miti katika kuleta mvua ambazo kwa kiwango kikubwa huchangia uwepo wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hivyo zoezi la leo lina uhusiano wa moja kwa moja na uwepo wa umeme wa uhakika nchini,” alifafanua Bi. Ndege.

Aidha, alisema kuwa matukio yote yanayofanyika ni muendelezo katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi 2023.

“Ndio sababu leo tumekuja wanawake wa TANESCO,  hususan wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kutekeleza shughuli hizi,” aliongezea Bi. Ndege.

Akitoa shukrani, Diwani wa kata Mfizi Yadhamicas Nghondo ameishukuru TANESCO kwa ufadhili wa huduma hizo muhimu kwa jamii kwani changamoto ya maji katika Kijiji cha nyani imekuwa ya muda mrefu, hali iliyokuwa inawalazimu wanafunzi na wanakijiji kufuata maji mto Ruvu umbali wa zaidi ya kilomita 5.

“Ni kweli kwamba shughuli za TANESCO ni kusambaza umeme na kuangazia maisha ya watanzania, lakini wamekuja kutuangazia maisha yetu kwa kutulekea hizi huduma tunawashukuru sana,” alisema Diwani Nghondo.

Mwaka 2019 na wwaka 2020 TANESCO kupitia wafanyakazi wake wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani walijenga vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na choo cha matundu 6. Jitihada hizo limesadia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo hadi kufikia zaidi ya asilimia 80 mwaka 2022.

TANESCO imeahidi kuendelea  kuboresha mazingira ya shule hiyo kwa kupaka rangi madarasa yaliyopo na kuboresha sakafu kwa madarasa yaliyochakaa.q
Posted by MROKI On Saturday, March 04, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo