Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2023








Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha siku ya Januari 7, 2023 Jijini Mbeya na kusababisha athari nyingi ikiwemo uharibifu wa miundombinu na mali za Wananchi.

Kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene leo Januari 11, 2023 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekadhi misaada hiyo kwa Uongozi wa Mkoa huo ikiwemo tani 50 za mahindi, magodoro 300, mablanketi 1200, mikeka 550, madumu ya maji 600, sufuria, vikombe, sahani n.k

Waziri Simbachawene baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika, amewaeleza Wananchi hao kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na maelekezo waliyopewa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuwataka kuboresha miundombinu ya Jiji hilo pamoja na kuwahudumia waathirika hao chakula kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amewataka Wananchi kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali yao ikiendelea na jitihada za kuwahudumia lakini pia amewatahadharisha kuepuka kujenga makazi katika maeneo ambayo sio rasmi na ni hatarishi.

Naye Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameishukuru Serikali kwa kuchukua hatua za haraka katika kuwasaidia Wananchi wake na zaidi ameiomba kulitazama kwa upekee Jimbo hilo ambalo limekuwa na changamoto nyingi za miundombinu.
Posted by MROKI On Wednesday, January 11, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo