RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika mnada wa Samaki katika Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023, akinadiwa Samaki aina ya Jodari na Dalali wa Soko hilo Bwa. Ali Hassan Mchoro, samaki huyo amebarikiwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi kwa shilingi 95,000/ katika mnada huo na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Yusushi Misawa, Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Makame, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zana Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akinunua Samaki katika Diko na Soko la Samaki Malindi Unguja Wilaya ya Mjini leo 10-1-2023, kwa mchuuzi Bwa. Khamis Hamad Omar, baada ya kufunguliwa Soko hili na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
WASANII wa Kikundi cha Ocean Art cha Mwanakwerekwe Unguja wakitowa burudani ya igizo la Uchumi wa Buluu wakati wa ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindizi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana, wakati wa Ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

MVUVI wa Diko la Malindi Unguja Bw.Suleiman Ali Seif (Mrusi) akishangilia kwa kupeperusha kipeperushi wakati wa ufunguzi Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia Wananchi na Wavuvi katika viwanja vya Soko la Samaki Malindi leo 10-1-2023, baada ya kulifungua ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi, Wavuvi na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika viwanja vya Soko la Samaki Malindi leo 10-1-2023, baada ya kulifungua ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment