Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Januari 09, 2023
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika
Januari 12, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Januari 09, 2023
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika
Januari 12, 2023.
***********
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwaongoza
wananchi wa Jiji la Dodoma kupanda miti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka
59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Januari 09, 2023 jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika Januari 12, 2023.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Jafo amesema kuwa Mhe. Makamu wa Rais ataongoza zoezi la upandaji miti katika maeneo ya Barabara ya Dodoma - Dar es Salaam, kuanzia Stendi kuu ya Dodoma (Nane nane) hadi Ihumwa pamoja na Shule ya Msingi Msalato.
Pia, amesema shughuli hiyo itatanguliwa na shughuli nyingine za upandaji miti Januari 10, 2023 katika maeneo ya pembezoni mwa barabara ya Dodoma – Dar es Salaam kuanzia chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) hadi Kilimo Kwanza ambayo itaongozwa na Waziri wa Dkt. Jafo.
Hivyo, amewataka Watanzania wote Bara na Zanzibar kupanda miti katika makazi yao na kuendelea kuitunza hadi ikue na kuongeza uoto wa asili katika nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment