Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
JESHI la polisi mkoani Iringa
linamshikilia David Richard (23) kwa kwa tuhuma za kuiba gari aina ya Raum
rangi ya Grey yenye namba za usajili T 702 DFV mali ya Gasper Abraham mwenye(34) aliloiba katika eneo lake la kazi
Akizungumza na waandishi wa
habari mkoani Iringa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan
Bukumbi amesema kuwa wamemkamata kijana huyo baada ya taarifa za kuibiwa kwa
gari hilo kutolewa na hivyo kupelekea jeshi la polisi kufanya doria ya kutosha
na kuikuta wilaya ya kilolo mkoani hapa
“Tunamshikilia David Richard (23) mlinzi wa RUCU aliiba gari hiyo ikiwa kwenye maegesho
lakini mmiliki alitoa taarifa kwenye jeshi la polisi na ndipo utaratibu wa
kumtafuta ukaanza ndipo ilipokutwa kwa mtuhumiwa akiitumia wilaya ya kilolo “
Pamoja na hayo Allan Bukumbi
alisema kuwa miongoni wa wahalifu waliofanikiwa kuwakamata
katika msako walioufanya walifanikiwa kumkamata ndugu Boni Kipalile
kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu
moja ikiwa chemba huku wakimshikilia Benadetha Kipago(61) akiwa na
meno ya tembo na kiboko
“Ndugu waandishi wa habari
kutokana na taarifa za siri kijiji cha kiponzero wilaya ya mkoa wa Iringa
tulifanikiwa kumkamata boni kipalile mkulima mkazi wa igangidungu anayetuhumiwa
kujihisuisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akizwa na silaha moja aina ya
shortgun namba za usajili 14949na risasi tatu moja ikiwa chemba pamoja na hilo
tunamshikilia benedetha kipago kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na meno
mawili ya kiboko “
Aidha kamanda wa Jeshi la
polisi mkoani Iringa amewataka wananchi kujitokeza na kutambua mali
zilizokamatwa kwa watuhumiwa Emmanuel Mnyeke (28) na Alfred Mkanula (25) ambao
walikamatwa na mali za wizi ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina ya sanlg ,boxer
na honda
Katika kushUghulikia
changamoto mbalimbali jeshi la polisi mkoani iringa lilifanikiwa kumkamata
Sebastian Mahuwili (42) aliyehukumiwa kwa kesi ya kubaka mtoto wa miaka 6 na
hivyo kupelekea Kufungwa miaka 30 jela kutokana na ushahidi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment