Nafasi Ya Matangazo

December 30, 2022


 

Posted by MROKI On Friday, December 30, 2022 No comments
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini Pretoria, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na wa pili kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika Kusini Balozi, Peter Shija.
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini  Pretoria, Desemba 30, 2022. wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika Kusini Balozi, Peter Shija
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini  Pretoria  Ijumaa Desemba 30, 2022. 
***********
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na watumishi katika balozi waendelee kufanya tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kupata kutokana na ushirikiano wa kidiplomasia kwenye nchi walizopo.

 

Amesema ni vema balozi hizo zikaanzisha majukwaa ya kiuchumi yatakayowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo ardhi, madini, utalii, mawasiliano na biashara.

 

“Muwasihi wafanyabiashara na wawekezaji waje kuwekeza Tanzania na washirikiane na Watanzania kufungua makampuni, hii itatusaidia Watanzania kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha biashara.”

 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 30, 2022) wakati akizungumza na watumishi wa ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Pretoria, Afrika Kusini.

 

Amesema watumishi wa balozi za Tanzania hawana budi kuandaa makubaliano baina ya Tanzania na nchi walizoko ambayo yataonesha nini kinatakiwa nchini humo na ambacho kinapatikana kwa wingi nyumbani Tanzania.

 

“Hapa kwenu, ubalozi unapaswa kutengeneza makubaliano maalum ya kibiashara miongoni mwa nchi hizi mbili na kubainisha aina ya bidhaa ambazo zinapatikana Tanzania kwa wingi na zinahitajika Afrika Kusini,” amesisitiza.

 

Aidha, Waziri Mkuu amesema ni vema pia ubalozi huo ukaendelea kuhamasisha watalii kutoka nchini humo kwa kubainisha vivituo vya utalii vilivyoko Tanzania ambavyo nchi hiyo haina huku akitolea mfano Mlima Kilimanjaro.

 

Awali, akitoa taarifa ya kiutendaji ya ubalozi huo, Kaimu Balozi Peter Shija alisema Tanzania inaweza kunufaika zaidi na fursa za biashara zilizopo nchini humo kwa kuuza mazao kama, mchele, maharage, korosho na mazao ya matunda.

Posted by MROKI On Friday, December 30, 2022 No comments
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wagonjwa waliokua wakisubiri matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala Mkoani Dar es Salaam.
Wagonjwa wakiwa ka mitika dirisha la dawa.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wagonjwa waliokua wakisubiri matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala Mkoani Dar es Salaam.
Na Englibert Kayombo, WAF - Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku ya kuendelea na ujenzi wa majengo mapya katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ambazo hazina mpango wa uendelezaji ardhi (Masterplan).

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam na kukuta ujenzi wa majengo ukiendelea ambayo hayajawekwa kwenye mpangilio mzurii wa  kutoa huduma zinazoendana pindi yatakapo kamilika.

"Nimepiga marufuku hapa Mwananyamala, hatutoweka jengo lolote bila ya kuwa na ‘Masterplan’ ya Hospitali, tukiwa na ‘Masterplan’ huduma pia zitakuwa zinaendana na zinapatikana kwa ukaribu” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema kwa hali iliyopo sasa wananchi wanatumia muda mwingi na kuzunguka kufuata huduma ndani ya Hospitali kwakuwa majengo ya kutolea huduma yamewekwa mbali mbali.

“Unaenda Maabara unaikuta iko peke yake, vipimo vya Xray vipo peke yake, UltraSound iko peke yake, tunataka kama ni masuala ya uchunguzi mgonjwa anakwenda kwenye jengo moja anapata huduma zote za uchunguzi” amefafanua Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesisitiza kuwa agizo hilo sio kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala bali ni la nchi nzima hususani kwa Hospitali zile za zamani ambazo zilijengwa bila ya kuwa na "Masterplan"
Posted by MROKI On Friday, December 30, 2022 No comments

December 29, 2022

Edson Arantes do Nascimento au maarufu Pele amefariki duania akiwa na umri wa miaka 82. 

Mchambuzi wa habari, rafiki yangu Maggid Mjengwa anaandika machache kuhusu kiumbe huyu gwiji wa kupachika mabao awapo uwanjani akilisakata gozinla Ng'ombe.

Anasema Pele, itakumbukwa, kuwa   ulimwengu wa kandanda ulishuhudia ujio wa mchezaji aliyekuwa na umri mdogo kuliko wengine wote katika fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 1958 kule nchini Sweden. Kijana huyu mdogo alikuwa na miaka 17 tu, aliitwa Pele.

Ni mchezaji huyu mdogo ambaye nyota yake iliyoanza kung'aa akiwa Sweden, ikaja kung'aa zaidi na kuacha simulizi zitakazodumu milele. Mchango wake ukaja pia kuibadili  soka ya dunia. 

Binadamu mwenzetu huyu ambaye ni maarufu kwa jina moja la Pele ana jina lake kamili ambalo ni refu kidogo. Anaitwa Edson Arantes do Nascimento.

Pele alizaliwa Oktoba 23 mwaka 1940. Kitu pekee kilichompambanua Pele kutoka kwa wachezaji wengine ni uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao.

Kulingana na taarifa rasmi, inaaminika, kuwa Pele amefunga magoli 1281 kati ya mechi 1363 alizopata kucheza. Huo ni wastani wa goli 0.9398 kwa kila mechi! Kwa hesabu hizo za kitaalam, hakuna mchezaji mwingine yeyote duniani aliyepata kukaribia rekodi hiyo.

Akiwa na timu ya taifa ya Brazil, Pele alipata kufunga magoli 77 kati ya mechi 92 alizocheza. Hiyo ni rekodi kwa taifa la Brazil, lakini si rekodi ya dunia. Rekodi ya dunia hadi sasa inashikiliwa na mchezaji Ali Daei wa Iran aliyepata kufunga magoli 104 akiwa na timu ya taifa ya nchi yake.

Labda tukio lililosubiriwa na wapenzi wengi wa kandanda ni lile la mchezaji huyo nyota  kufunga goli lake la 1000. Goli hilo lilifungwa na Pele katika mechi yake ya 909 mnamo mwaka 1969.
Alilifunga kwa penalti  akiwa na klabu yake ya Santos.

Mwaka 1959 utakumbukwa kama mwaka ambao Pele alipachika nyavuni  magoli mengi zaidi kuliko miaka mingine yote akiwa mchezaji.
Katika mechi zote za mwaka huo, Pele alipachika  jumla ya magoli 126.

Pele hakuwa tu sumu kali katika kufunga magoli, Pele aliogopewa na timu pinzani pia. Alikuwa hodari karibu kwa kila kitu alipokuwa uwanjani. Alikuwa na ufundi mkubwa. 

Pele alikuwa na  uelewa mkubwa wa mchezo. Aliweza kupiga mashuti makali kwa miguu yote miwili na alikuwa hodari kwa kupiga mipira ya adhabu ndogo. 

Pele huyu alikuwa hodari pia kwa kutoa pasi "zenye macho". Pasi zake zilikuwa za uhakika kana kwamba alifunga pimamaji miguuni. 

Ingawa Pele hakuwa mrefu sana, lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya juu. Aliweza kuruka na kuipata mipira mingi ya vichwa.
 

Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2022 No comments
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Jerry Mwaga (wa tatu kutoka kulia), akiwa na Viongozi wenzake katika moja ya harakati za utekelezaji shughuli za maendeleo, wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ulyankkulu liliko Wilayani humo Rehema Migira akifuatiwa na Mbunge wa Jimboa la Kaliua Aloyse Kwezi na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo Japhael Lufungija ( wa nne kulia).
 
************
Na Lucas Raphael,Tabora
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua Mkoani hapa imedhamiria kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula ya alizeti kwa kuwezesha vikundi vya wakulima katika kata zote mbegu za kutosha za zao hilo ili kuanza kilimo hicho.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Jerry Mwaga alipokuwa akizungumza na gazeti hii Ofisini kwake ambapo alisema kwa kuanzia wamesambaza jumla ya kilo 6,650 za mbegu za alizeti katika kata 16.

Alitaja kata ambazo zimepata mbegu hizo kuwa ni Ukumbisiganga, Zugimlole, Ushokola, Ugunga, Kazaroho, Igagala, Usenye, Usinge, Kamsekwa, Ichemba, Mwongozo,Sasu, Ilege, Ufuutwa, Igwisi, Uyowa na Kona nne.

Alibainisha kuwa zoezi la usambazaji mbegu hizo litakuwa endelevu ili kuhakikisha wakulima wa wilaya hiyo wanakuwa na zao mbadala wa tumbaku litakalowaingizia mapato mazuri na kuwainua kiuchumi.

Aliongeza kuwa ili kuwa na kilimo chenye tija kitakachowanufaika wakulima na jamii kwa ujumla wameweka utaratibu wa kutoa elimu kwa vikundi vyote vya uzalishaji mali wilayani humo.

Alifafanua kuwa ili kuboresha shughuli za kilimo katika wilaya hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu imewajengea kitalu-nyumba kitakachotumika kutolea mafunzo ya kilimo bora, hivyo akatoa wito kwa wakulima kuchangamkia fursa hiyo.

‘Tumedhamiria kuongeza uzalishaji wa mazao chakula na biashara ili kuwainua zaidi wakulima wetu, hadi sasa jumla ya vijana 97kutoka maeneo mbalimbali wamepatiwa mafunzo na zoezi bado linaendelea’, alisema.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jafael Lufungija alisema licha ya kugawiwa mbegu mkakati wa halmashauri hiyo ni kuhakikisha vikundi vyote vya akinamama, vijana na watu wenye ulemavu vinavyojishughulisha na uzalishaji mali vinawezeshwa mikopo nafuu ili kufanikisha shughuli zao.

Aliongeza kuwa halmashauri imetenga kiasi cha sh mil 107kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vyote vinavyojishughulisha na uzalishaji wa mafuta ya alizeti, mawese, utengenezaji viatu, chaki na sabuni.

Aidha alisema sh mil 17 zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha vikundi 2 vya wanawake vinavyojishughulisha na uchakataji asali na mazao mengine ya nyuki.
Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2022 No comments
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wananchi wa Wilaya ya Makete, Mkoani Njombe, kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani Makete.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw,Antony Mtaka, akiwasilisha taarifa ya Mkoa huo kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, iliyofanyika Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Mbunge wa Makete Mhe. Festo Sanga akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Makete kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, iliyofanyika Wilayani Makete, Mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw, Antony Mtaka, kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani hapo, Mkoani Njombe.
Sehemu ya Viongozi wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, iliyofanyika Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila akiwa na Muwakilishi wa Kampuni ya M/S China National Aero-Technology Engineering Corporation (wa pili kulia) wakionyesha mkataba wa Ujenzi wa Barabara  ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, mara baada ya kuusaini Wilayani Makete, Mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wakala wa Barabaraa Nchini (TANROADS) mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani Makete, Mkoani Njombe
*****************
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara za lami  katika mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuunganisha vema ukanda huo na bandari ya Mtwara na hivyo kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji, kukuza uzalishaji wa mazao ya kilimo, misitu na kukuza utalii.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa barabara ya Isyonje-Kikondo hadi Makete KM 96.2 sehemu ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya sita itahakikisha inaunganisha kwa njia fupi mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Njombe hadi Mbeya kupitia Makete ili kukuza fursa za kiuchumi zilizoko katika ushoroba huo.
 
  “Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imejikita kwenye kuboresha miundombinu hususani maeneo yenye uzalishaji mkubwa hivyo niwahakikishie kuwa ongezeni uzalishaji miundombinu bora inakuja,’ amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
 
Ameitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumsimamia kikamilifu Mkandarasi anayejenga barabara hiyo M/S China National Aero-Technology Egineering Corporation ili mradi huo ukamilike kwa wakati na viwango.
 
Mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila  amesema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa mizani katika Kijiji cha Igalala ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kulinda miundombinu yote ya barabara.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Makete Festo Sanga ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo kwani kukamilika kwake kutaunganisha wilaya hiyo na Mkoa wa Mbeya kwa njia fupi, kukuza utalii wa hifadhi ya taifa Kitulo na kupandisha thamani ya mazao mbalimbali yanayozalishwa Mkoani Njombe.
 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Bw, Anthon Mtaka amewataka wakazi wa wilaya ya Makete kote nchini kutumia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu kuwekeza wilayani humo.
 
Zaidi ya shilingi bilioni 69.7 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 36. 
Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2022 No comments

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo,Amani Mashaka wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Msajili wa Jumuiya za Kiraia,Emmanuel Kihampa wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani,Martina Nguluma  wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Juma Mnyanile  wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Mariamu Omary wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.

Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2022 No comments


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.
Wageni mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili  yaani” Doctor of Philosophy in Kiswahili” Nunuu Abdalla Mohammed, wakati wa hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Teknolojia ya Habari yaani  “Bachelor Degree of Information Technology Application and Management” wakati wa hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Leila Mohammed Mussa.
Wahitimu wa Shahada ya Utabibu yaani “ Doctor of Medicine” Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakila kiapo cha Utii na Uadilifu wa kazi yao, baada ya kutunukiwa Shahada ya Utabibu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika Mahafali ya 18 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.
Wahitimu wa Cheti cha Uongozi wa Fedha yaani ”Certificate in Financial Administration” wakishangia baada ya kutunukiwa Cheti katika Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-112-2022.


Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2022 No comments

December 28, 2022

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Regina Lowassa mke wa Waziri Mkuu Mstaafu (wa tatu kushoto) na Fredrick Lowassa (kulia) alipoenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa anayepata matibabu jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, Desemba 28, 2022. Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya  Kusini.
 
Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.
 
Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.
 
Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.
 
Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.
Posted by MROKI On Wednesday, December 28, 2022 No comments
 
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf katika kjiji cha kipanga Mlimani wakimsikiliza mwezeshaji wa Tasaf hayupo pichani
Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa Tasaf Josephine Mzoo akifanya  uhawilishaji kwa mmoja ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf
Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa walengwa wa Tasaf Josephine Mzoo wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha kipanga mlimani akizungumza na walengwa hao
Na Lucas Raphael,Tabora
Walengwa wa Tasaf wilayani sikonge mkoani Tabora wameshauriwa kulima mazao yanayo stahimili ukame kulingana na kuwepo kwa mvua kidogo inayoratajia kunyesha msimu huu wa kilimo.
 
Wito huo umetolewa jana na Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa walengwa wa Tasaf Josephine Mzoo wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha kipanga kata ya kipanga Mlimani wilayani Sikonge mkoani hapo.
 
Alisema kwamba wakulima wanapaswa kulima mazao kinga njaa ambayo ni Viazi na Mihogo ili kuweza kukabilia na njaa inayoweza kujitokeza katika msimu wa kilimo mwaka huu .
 
Josephine aliendelea kusema kwamba mvua za mwaka huu ni chache kulingana na utabiria wa hali ya hewa unaonyesha kuwa mvua zitanyesha chini ya wastani.
 
Naye mlengwa wa Tasaf katika kjiji cha Kipanga mlimani na kata ya Kipanga Nelea Katumbo alisema kwamba watajitaidi kulima mazao yanayostamili ukame ili kuweza kupata chakula katika msimu huu wa kilimo .
 
Alisema kwamba licha ya kulima mazao hayo pia amefanikiwa kufunga kuku na kisha kuweza kununua mbuzi na sasa ana mbuzi 11 ambao analengo la kuunza a kununua Ng’ombe.
Alisema kwamba toka kujiunga na mfuko huo amefanikiwa  kimaisha kwa kuweza kujiudumia kwa chakula ,kuweza kumudu kulima mazao mbalimbali kwa pesa anayopata, anatoa pesa nyingne kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi na chakula inayobaki kwa ajili ya mbole kwa ajili ya shamba .
Alisema kwamba licha ya kutumia mbole ya samadi kwenye mashamba lakini pia anatumia mbole ya madukani kwa ajili ya kupata mazao bora.
 
Naye Zafarani Hussein  alisema kwamba kulingana utabiri wa hali ya hewa unaosema mvua za mwaka huu zitanyesha chini ya wastani jambo ambalo wanalazimika kulima mazao  yanayostahimili  ukame.
 
Alisema ushauri huo ulitolewa na afisa kilimo wanauchukuwa kwa jicho la Tatu kutokana na mvua kunyesha kwa kiwango kidogo ila watajitaidi kuyatunza mazao ambayo tayari wameyapanda .
 
Hata hivyo malengo hayo amekiri kunufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini – Tasaf kwa kuweza kusomesha watoto, kuanzisha miradi kufunga mbuzi ,kuku, bata na  Ngombe.  
 
Alisema kuwa tangu ajiunge na TASAF  ambapo kwa mwaka huu ameweza kulima na anatarajia kupata  gunia 8 za mahindi, lengo ni kuongeza kulima mazao ya kilimo hasa  Karanga, Muhogo na kuongeze idadi ya kutoka mbuzi 10 hadi kununua  Ng’ombe wa  3 kwa ajili ya kumsaidia kulima mashamba yake .
 
Alisema kwamba licha ya kununua Ng’ombe hao pia amenunua jembe la kukokotwa na Ng’ombe kitu ambacho kitamsaidia kulima mashamba makubwa kikubwa kuona mvua inayesha vizuri .
 
“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuondolea umaskini huku vijijini kwetu, kama sio fedha hizo mimi ningekuwa nimeshakufa,  lakini kutokana na fedha hizo zimemsaida kimaendeleo”alisema Zafarani Husein  
  
Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya Jamii wilaya ya sikonge’   Claud Nkanwa Alisema walengwa wameendelea kupewa mafunzo ya kujiwekeza katika raslimali zalishi ili pindi mpango huo utakapoisha au kipindi chao kitakapoisha waweze kujiwezesha kuendelea na Maisha yaliyo bora .
 
Hata hivyo aliwataka wananchi wanaonufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini TASAF kuzitumia fedha hizo kama ambavyo wamekuwa wakifundishwa na viongozi wa TASAF huku akisema yeye atakuwa mfuatiliaji wa fedha hizo.

Posted by MROKI On Wednesday, December 28, 2022 No comments
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati alipozungumza na wananchi wa Kyela (hawapo pichani) katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4), mkoani Mbeya.
Mbunge wa Kyela Mhe. Ali Mlagila Jumbe akisisitiza jambo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), uliosainiwa katika Viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila (Kulia) na Muwakilishi wa Kampuni ya AVM-Dilingham Construction International Incorporated ya Nchini Uturuki mara baada ya kusaini Mkataba kwa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.

Sehemu ya wanachi wa Wilayani Kyela wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa( hayupo pichani) wakati alipozungumza nao katika hafla ya utiaji saini  mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4), katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini  mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4), Uliosaniwa katika Viwanjavya shule ya Msingi Mpanda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara, Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Kyela Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini  mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda-Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi (KM 4), uliosaniwa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.
***********
Serikali imesema itaendelea kutekeleza Sera yake ya kuunganisha mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya kwa barabara za lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria, mazao na malighafi mbalimbali ili kukuza uchumi kwa haraka.
 
Akizungumza wilayani Kyela wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ibanda hadi Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa  amesema kukamilika kwa barabara hizo kutaimarisha shughuli za kiuchumi kwa  wakazi wa wilaya za Rungwe na Kyela, na mikoa ya Ruvuma, Njombe na nchi jirani ya Malawi.
 
“Katika ukanda huu kuna malighafi na mazao ya kilimo,uvuvi na makaa ya mawe mengi yanayohitaji miundombinu rafiki kwa ajili ya kuwafikia watumiaji kwa wakati, ndio maana Serikali ya awamu ya sita imeamua kujenga barabara hizi kwa pamoja,’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.
 
Waziri Prof. Mbarawa amewataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kumsimamia vizuri  Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili azingatie viwango na thamani ya  fedha kulingana na mikataba.
 
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Kyela kuwa TANROADS itafanya uthamini upya ili kuhakikisha wananchi wanaopisha ujenzi wa barabara hizo wanapata stahili zao kwa mujibu wa sheria.
 
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema Kampuni ya AVM Dillingham Construction International Incorporated ya Nchini Uturuki imeshinda zabuni ya kujenga barabara hiyo na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 kuanzia sasa.
Zaidi ya shilingi bilioni 38 fedha za ndani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ambao pia utahusisha taa za barabarani.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya juma homera amewataka wananchi wa kyela kutumia fursa za ajira zitakazojitokeza wakati wa mradi huo kufanyakazi kwa bidii na uzalendo ili kuwezesha maradi huo kukamilika kwa wakati.
 
Kwa upande wake Mbunge wa ileje ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa barabara wilayani kyela ni muendelezo wa mkakati wa serikali katika kuhakikisha barabara zote za nyanda za juu kusini zinazopiyta maeneo ya uzalishaji zinakuwa katika viwango bora na hivyo kutumika wakati wote na kuongeza tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Posted by MROKI On Wednesday, December 28, 2022 No comments

December 27, 2022

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim (Katikati) wakati alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es salaam Disemba 27, 2022. Kushoto ni Ahmed Salim ambaye ni Mtoto wa Dkt. Salim
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ahmed Salim ambaye mtoto wa  Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati alipomtembelea Waziri Mkuu huyo Mstaafu nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es salaam Disemba 27, 2022.

 

Posted by MROKI On Tuesday, December 27, 2022 No comments
Adeladius Makwega
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abel Philip amekabidhi gari aina ya Toyota Coaster lenye namba ya usajili STM 2639 kwa MkurugenzI Msaidizi wa Utawala na Rasimali Watu, Zahara Guga Desemba 27, 2022 Jijini Dodoma kwa shughuli kadhaa za utendaji.
 
Akizunguma katika makabidhiano hayo Kaimu Katibu Mkuu Philip, amesema kuwa gari hiyo iliyonunuliwa kwa shilingi milioni 236, 213, 589.29/- itatumika katika kuboresha utendaji kazi wa wizara na kuwafikia wadau wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.
 
“Ninakabidhi chombo hiki kikiwa imara na ubora wake, matarajio ya serikali Idara ya Utawala na Rasilimali watu itahakikisha gari hili linatunzwa na wanaoliendesha na wanaolipanda kwa nyakati tofauti, litumike ipasavyo katika kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa ili tukamilisha malengo ya ununuzi wake na kutunza mali za umma,” alisema Philip.
 
Aidha, akizungumza mara baada ya kulipokea basi hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bi Zahara Guga amemuhakikishia Kaimu Katibu Mkuu kuwa gari hilo litatunzwa vizuri kama ilivyokusudiwa.


Posted by MROKI On Tuesday, December 27, 2022 No comments
Diwani wa Kata Nsololo Habibu Sungwa Alipokuwa Akishuudia matofali ya kuchoma  aliyevaa shati la kijivu alivaa shati la maua ni Mratibu wa Tasaf wilaya ya Uyui mkoan hapa Dkt Kija Maige .
Bi Asia Hamad akiwa ameshikili moja ya matofali ya kuchoma
Mlengwa wa Tasaf Fatuma Habibu akiwa amejipomzisha nyumbani kwake
Mratibu wa Tasaf wilaya ya Uyui mkoan hapa Dkt Kija Maige aliyevaa shati la kitenge akisisitiza jambo kwa walengwa wa mapnga wa Tasaf katika kata ya Nsololo wilaya ya Uyui Tabora 
***********
 Na Lucas Raphael
Walengwa wanaonufaika na mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF katika kata ya Nsololo wilaya y uyui Mkoani Tabora wametakiwa kuacha  kutumia fedha wanazopatiwa na serikali kufanya matendo ya anasa badala yake kujiwekea akiba na kuwawezesha  kujiinua kiuchumi.
 
Kauli hiyo jana ilitolewa jana na Diwani wa Kata Nsololo Habibu Sungwa alipokuwa akizungmza na walengwa hao wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha Nsololo kata ya Nsololo wilayano humo .
 
Alisema kwamba fedha wanazozipata wazitumia kwa kujengea uwezo wa kubuni miradi mbaimbali ya maendeleo na sio kutumia fedha hizo kwa anasa jambo ambalo halina tija kwao na familia zao.
 
Alisema kwamba lengo la serikali kupitia Tasaf ni kujengea uwezo wananchi wake kwa kuondokana na umaskiniwa kipato na kuwafanya kuwa jamii yenye  mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
 
Diwani huyo alisema kwamba walengwa wa mfuko huo wanatakiwa kuiga mfano wa Fatuma Habibu ambaye ameweza kuwa na benki ya matofali licha ya hali yake ya kiafya kuwa sio nzuri lakini ameweza kufunga kuku 25 hadi kuwa na Mradi wa tofali za kuchoma 3500 .
 
Mlengwa wa Tasaf Fatuma Habibu ambaye anasumbuliwa na maumivu makali ya miguu kiasi cha kushindwa kutembea na kusimama kwa muda mrefu alisema kwamba licha ya hali yake hiyo bado anapambana kwa ajili ya kujiinua kiuchumi akishirikia na  watoto wake .
 
Alisema kwamba amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa mwanaye huyo ambaye amekuwa nguzo ya kuweza kumsaidia katika shughuli mbali mbali alizokuwa anapaswa kufanya mama huyo.
 
"anashukuru sana kwa kazi kubwa anayoifanya kijana wangu hadi kufikia hapo alipofika sasa ambapo kila kitu mwanaye huyo ndiye anayefanya kutokana na yeye kupata maradhi ya miguu kumuuma kwa kipindi kirefu sasa' anasema Fatuma
 
Naye mwanae Asia Hamad alisema kwamba toka wajiunge ana mango wa kunusuru kaya masikini wamekuwa na masha mazuri tofauti na kipindi cha nyuma .
 
Alisema wkwamba fedha ambazo wamekuwa wakizipata wamekuwa wajitaidia kuanzisha miradi tofauti Tofauti hadi kufikia kuwa na benki ya matofali ambayo wanauza kwa ajili ya kuongeza kipato .
 
Alisema kwamba licha ya wao kujiongezea kipato pia wanaajiri watu wengine ka ajili ya kufetua matofali kwani wao pekee yao hawezi ila kwa kushirikiana na jamii wanafanikiwa.
 
Asia alisema kwamba lengo lao mwaka huu ni kulima mazao mbalimbali ikiwemo Alizeti Eka 4 karanga Eka 2,Viazi ,2 na mihogo 2 wanafanya hivo kutokana na uhitaj wa mvua.
 
Anaye mratibu wa Tasaf wilaya ya Uyui mkoan hapa Dkt Kija Maige aliwataka walengwa hao kutumia raslimali zilizopo kwenye maeneo yao kwa ajili ya kujiletea maendeleona kujiinua Kiuchumi.

Katika TASAF Awamu ya Tatu Kipindi cha Pili katika wilaya ya Uyui inahudumia zaidi ya vijiji 150, ukiwalenga wale wenye umri kati ya miaka 18 hadi 65 wenye nguvu za kufanya kazi pamoja na wazee wenye umri kuanzia miaka 66 na kuendelea.

Posted by MROKI On Tuesday, December 27, 2022 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo