Nafasi Ya Matangazo

December 27, 2022

Adeladius Makwega
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abel Philip amekabidhi gari aina ya Toyota Coaster lenye namba ya usajili STM 2639 kwa MkurugenzI Msaidizi wa Utawala na Rasimali Watu, Zahara Guga Desemba 27, 2022 Jijini Dodoma kwa shughuli kadhaa za utendaji.
 
Akizunguma katika makabidhiano hayo Kaimu Katibu Mkuu Philip, amesema kuwa gari hiyo iliyonunuliwa kwa shilingi milioni 236, 213, 589.29/- itatumika katika kuboresha utendaji kazi wa wizara na kuwafikia wadau wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.
 
“Ninakabidhi chombo hiki kikiwa imara na ubora wake, matarajio ya serikali Idara ya Utawala na Rasilimali watu itahakikisha gari hili linatunzwa na wanaoliendesha na wanaolipanda kwa nyakati tofauti, litumike ipasavyo katika kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa ili tukamilisha malengo ya ununuzi wake na kutunza mali za umma,” alisema Philip.
 
Aidha, akizungumza mara baada ya kulipokea basi hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bi Zahara Guga amemuhakikishia Kaimu Katibu Mkuu kuwa gari hilo litatunzwa vizuri kama ilivyokusudiwa.


Posted by MROKI On Tuesday, December 27, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo