Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar-es-salaam.
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika” utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye ataufungua rasmi mkutano huo tarehe 12 Septemba 2022 katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano (JNICC), Dar es Salaam.
Mkutano huo utahudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mabalozi, Mawaziri wa Biashara na Mawaziri wa masuala ya jinsia.
Mkutano huu pia utawakutanisha, Wanawake na Vijana wanaojishughulisha na masuala ya biashara, watunga sera, wafadhili, wadau wa maendeleo, na wadau wengine muhimu wa biashara barani Afrika ambao watajadili kwa kina agenda Wanawake na Vijana katika biashara barani Afrika.
Viongozi Wakuu walioawasili nchini na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ili kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo.
0 comments:
Post a Comment