Nafasi Ya Matangazo

September 16, 2022

Patricia Kimelemeta
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amewataka wazazi na walezi kuzingatia mwongozo wa Malezi, makuzi na maendeleo ya Awali Kwa watoto (PJT-MMMAM)  ndani ya Siku 1000 ili waweze kuwa na afya bora na kukuza ubongo jambo ambalo litasaidia kupunguza udumavu Kwa watoto.

Gondwe alisema hayo kwenye uzinduzi wa PJT-MMMAM ngazi ya Mkoa ambapo Kila Halmashauri inapaswa kutekeleza afua zilizopo kwenye Programu hiyo Hadi Mwaka 2026.

Programu hiyo inatoa maelekezo ya Malezi, makuzi na maendeleo ya Awali ya Mtoto kuanzia umri sifuri Hadi miaka minane jambo ambalo litaweza kupunguza udumavu, ukatili na watoto kupata Malezi yenye mwitikio.

Alisema kuwa, kuongezeka ka udumavu ka watoto wachanga ni miongoni mwa sababu za watoto kukosa Malezi Bora na lishe duni, jambo ambalo ni hatari Kwa Taifa Kwa sababu wanaweza kizalisha viongozi wasio na fya Bora, hivyo basi wakati umefika wa Kila Mwananchi kuzingatia Malezi Bora Kwa watoto.

Alisema kuwa, Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe(TFNC) zinaonyesha kuwa, Dar es Salaam ni Mkoa wa tatu kuwa na watoto wenye udumavu ikiongozwa na Kagera Kigoma.

" Tuna Kila sababu ya kutoa elimu kwa jamii Ili waweze kuzingatia lishe bora Kwa watoto hasa walio ndani ya Siku 1000 Ili kuzalisha taifa Bora lenye viongozi imara waliopata Malezi yenye mwitikio na kukuza ubongo wao, jambo ambalo litapunguza vjtwndo vya ukatili, mmonyoko wa maadili na unyanyasai," alisema Gondwe.

Aliongeza kuwa kutokana na Hali hiyo, Programu hiyo itasaidia kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa lishe Bora, ujifunzaji wa awali, michezo na hata kupunguza vitendo vya ukatili Katika jamii.

" Ikiwa mtoto atapata Malezi bora kuanzia kwenye uangalizi Hadi lishe Bora, tutazalisha Taifa imara ambayo litakua na viongozi Bora, hivyo basi kuzinduliwa kwa Programu hii kutasaidia kupunguza changamoto zilizopo," alisema Gondwe.

Aliongeza kuwa, Ili kuhakikisha watoto hao wanalelewa Katika mazingira Bora, Serikali ya Mkoa wa Dar Es Salaam imezitaka halmashauri zote kutekeleza afua za Malezi na makuzi Ili kuhakikisha watoto walio chini ya Miaka minane waweze kukua Katika mazingira Bora.
Posted by MROKI On Friday, September 16, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo