1. Waziri wa ElLmu, Sayansi na Teknolojia, Prof.
Adolf Mkenda (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji
Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023.
Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru na Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi HESLB, Prof. Hamisi Dihenga. Hafla hiyo imefanyika leo
Jumanne Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
Uombaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la
Posta (TPC), Macrice Mbodo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu
kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Prof. Hamisi Dihenga akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka
wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHELB) akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Mwongozo wa Uombaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo
2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi kutoka Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao ni wadau wa kimkakati wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi wa mwongozo
wa uombaji mikopo kwa mwaka 2022/2023. (Picha zote na HESLB)
***************
Na Mwandishi Wetu, Dar es
salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewahimiza waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa
mwaka 2022/2023 kusoma na kuuzingatia ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa 2022/2023’
ili kuwasilisha maombi kwa usahihi.
Prof. Mkenda ameyasema hayo katika
hafla fupi ya kuzindua mwongozo huo iliyofanyika katika ofisi za HESLB jijini
Dar es salaam na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. James Mdoe, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa HESLB Prof.
Hamisi Dihenga na wadau wengine wa HESLB.
Prof. Mkenda amesema: “Kuanzia
leo (Jumanne, Julai 12), mwongozo huu utapatikana katika tovuti ya HESLB
(www.heslb.go.tz) na ya Wizara (www.moe.go.tz) katika lugha mbili za Kiswahili
na Kiingereza … na kuwapa fursa waombaji kuusoma. Dirisha la kupokea maombi ya mikopo kwa njia
ya mtandao linatarajiwa kufunguliwa Julai 19 hadi Septemba 30, 2022,” amesema
na kuongeza:
“Dirisha la maombi ya mikopo
kwa mwaka wa masomo 2022/2023 litakuwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19
hadi Septemba 30 mwaka huu, hivyo tunawasihi wanafunzi waombaji wasome mwongozo
kabla ya kuomba mkopo kwa kuwa ndiyo unataja sifa, vigezo na utaratibu wa
kuomba mkopo,” amesema Prof. Mkenda.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe
amewakumbusha waombaji mikopo kuzingatia maelekezo yaliyomo kwenye mwongozo ili
kuondokana na changamoto ambazo hujitokeza kwa waombaji.
“Uzoefu unaonesha kuwa
wanafunzi waombaji wamekuwa hawazingatii taratibu wakati wa kufanya maombi.
Tunawasii mzingatie maelekezo ya mwongozo. Wakati wa dirisha la maombi
kumekuwepo na changamoto nyingi zinazojitokeza kwa waombaji”, amesema Prof.
Mdoe.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema kila mwaka mwezi Julai, HESLB huanza kupokea
maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo unaofuata ambapo mwongozo huo hutoa maelezo
ya kina kuhusu sifa na utaratibu wa kupanga mikopo kwa mwaka husika.
“Mwongozo huo umekamilika na
kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi. Kuanzia wiki ijayo, tutaanza kuendesha
programu za elimu kwa umma kupitia redio, televisheni, mikutano katika Kambi za
JKT na mitandao ya kijamii” amesema Badru.
0 comments:
Post a Comment