CHAMA cha Wasafirishaji
Tanzania (TAT) kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia
Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kusikiliza na kufanyia kazi maoni ya
Wasafirishaji nchini kwenye Bajeti ya Mwaka 2022/2023.
Taarifa kutoka Ofisi ya Rais
wa TAT, Mohammed Abdullah, ya mwishoni mwa wiki, imesema: “Kwa niaba ya Chama
cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Bodi, Wanachama na Wasafirishaji wote nchini,
tunapenda kukupongeza Mh.Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na wasaidizi wako kwa kuwasikiliza Wasafirishaji wa
mizigo katika Bajeti ya Mwaka 2022/23.
Tunayo furaha kubwa kukupa
pongezi za dhati kabisa pamoja na wataalamu wako ambao wamekuwa wakifanya kazi
nzuri kuishirikisha Sekta Binafsi katika masuala mbalimbali ya Bajeti na Kodi.
“Tunashukuru sana kwa punguzo
katika Kodi ya Matrela na Vichwa vya Magari ya kusafirishia mizigo hadi 0%, na
Punguzo katika Tozo ya matumizi ya barabara kutoka dola za Marekani 16 kwa
kilomita 100 hadi dola 10 kwa kilomita 100.
Tunakupongeza Rais Mama Samia
Suluhu Hassan na Serikali yako kwa kuwa sikivu kwa maombi ya Wasafirishaji
nchini na tuna imani kubwa kuwa changamoto ambazo hazijatatuliwa, zitafanyiwa
marekebisho ili zilete tija katika Sekta ya Usafirishaji na
nchi kwa ujumla.”
TAT ni chama chenye wanachama
wasafirishaji wa mizigo na mafuta zaidi ya 200 nchini. Changamoto katika Sekta
ya Usafirishaji zinawagusa moja kwa wanachama wake na Wasafirishaji wote
nchini.
0 comments:
Post a Comment