Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, amejumuika na Wananchi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Husein Ali Mwinyi, katika maziko ya Baba wa Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Shaibu Hassan Kaduara.Marehemu Mzee Hassan Kaduara, amefariki dunia usiku wa Juni 17, nyumbani kwake Fuoni Mambosasa na kuzikwa leo June 18, katika makaburi ya Mwera Pongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi Amin!








0 comments:
Post a Comment