Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wengine pichani ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemad Suleiman Abdulla (wa pili kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamad Mussa (kushoto), Mwenyekiti na Muanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF), Mhe. Wanu Hafidh Ameir pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Mhe. Fatma Mwassa.

Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein mara baada ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Wanu Hafidh Ameir akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi, Wanafunzi na Wananchi alipowasili katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022 kwa ajili ya kuzinduzia Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi na Wananchi baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.











0 comments:
Post a Comment