Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman akizungumza na Balozi mdogo wa Uingereza Nchini Tanzania Bwn. Rick Shearn (kulia kwake) aliyefika na ujumbe wake kwaajili ya maongezi na mashauri ya mambo mbalimbali ya Maendeleo, kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza Migombani- Zanzibar leo Juni 17,2022.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman akisakimina na Balozi mdogo wa Uingereza Nchini Tanzania Bwn. Rick Shearn .
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza na ujumbe wa Kamati ya Michezo kwaajili ya watu wenye ulemavu wa Akili Zanzibar (SOZ), waliofika ofisini kwake Migombani- Zanzibar kwaajili ya kubadilishana mawazo na kukabidhi Medali walizopata kutoka katika mashindano mbalimbali, anayekabidhi Medali ni Mkurugenzi wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar ,Ndg. Ussi Haji Debe, Juni 17,2022.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema mageuzi makubwa katika Mfumo wa Chaguzi na uwepo wa Tume Maalum ya Kusimamia Maridhiano ya Kisiasa Nchini, kwamba ni mambo yasiyoweza kuepukika kwa sasa hapa Visiwani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman akisakimina na Balozi mdogo wa Uingereza Nchini Tanzania Bwn. Rick Shearn .
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza na ujumbe wa Kamati ya Michezo kwaajili ya watu wenye ulemavu wa Akili Zanzibar (SOZ), waliofika ofisini kwake Migombani- Zanzibar kwaajili ya kubadilishana mawazo na kukabidhi Medali walizopata kutoka katika mashindano mbalimbali, anayekabidhi Medali ni Mkurugenzi wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar ,Ndg. Ussi Haji Debe, Juni 17,2022.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema mageuzi makubwa katika Mfumo wa Chaguzi na uwepo wa Tume Maalum ya Kusimamia Maridhiano ya Kisiasa Nchini, kwamba ni mambo yasiyoweza kuepukika kwa sasa hapa Visiwani.
Mheshimwa Othman ameyasema hayo leo, Ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar akizungumza na Balozi Mdogo wa Uingereza Nchini Tanzania, Bw. Rick Shearn, aliyefika na Ujumbe wake kwaajili ya maongezi na mashauri juu ya mambo mbali mbali ya maendeleo.
Amesema hayo ni kutokana na ukweli kwamba Tume za Uchaguzi ziliopo sasa zimeshindwa kuijengea Nchi mazingira bora ya siasa, uongozi na maendeleo, na kinyume chake ni kuendeleza changamoto zikiwemo za machungu na maonevu yanayojirudia mara kwa mara dhidi ya wananchi.
“Tunachokihitaji sasa ni Tume huru ya Uchaguzi inayokubalika kwani iliyopo sasa imegubikwa na changamoto nyingi ambapo pamoja na kujiona ipo sahihi kwa kila jambo na haitendi makosa lakini malengo na mipango yake yamekuwa kikwazo cha maendeleo na maisha ya wananchi kwa ujumla”, amesema Mheshimiwa Othman.
Hivyo amesema mabadiliko yanayohitajika ambayo ni sehemu ya hoja zake za msingi mbele ya Kikosi-Kazi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachoratibu maoni juu ya mwenendo wa kisiasa Nchini, ni msingi wa maisha na ustawi bora wa jamii, siasa za kistaarabu, uvumilivu na hatimaye umoja wa kitaifa.
Kuhusu usimamizi wa maridhiano ya kisiasa nchini, Mheshimiwa Othman amesema kuwa ufanisi unaweza kufikiwa pindipo ikiundwa Tume Maalum, itakayozingatia uwiano, ridhaa ya wananchi, uongozi wenye ufanisi na kutanguliza maslahi ya Taifa.
Ameeleza kuwa Muundo wa Tume kama hiyo uliwahi kushuhudiwa hapa Visiwani kupitia Maridhiano ya Kisiasa yaliyotangulia, ambayo iliongozwa kwa ridhaa, Uenyekiti wa pamoja na uwakilishi sawasawa wa Wajumbe wake, ikihusisha Chama Tawala na Upinzani, ambapo miongoni mwa mafanikio yake muhimu ni kufanikisha mwamko na uelewa mkubwa kwa umma.
Kwa upande wake Balozi Shearn, amesema lengo la Serikali ya Uingereza ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Maridhiano ya Kisiasa pamoja na mwenendo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, sambamba na kujaribu kusaidia mazingira ya kufanikisha mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Visiwani na Tanzania kwa ujumla.
Ametaja sekta mbali mbali ambazo Serikali ya Uingereza inadhamiria kuzijengea uwezo zikiwemo utekelezaji wa Sera za Kupambana na Dawa za Kulevya, Uhifadhi wa Mazingira na Makabiliano ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, Utekelezaji wa Maridhiano, Umoja wa Kitaifa Zanzibar, na ujenzi wa mifumo bora ya mageuzi ya kisiasa.
Katika ujumbe wake Balozi Shearn, ameambatana pia na Afisa Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bw. Graeme Bannatyne.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Othman amekutana na kubadilishana mawazo na Kamati ya Michezo kwaajili ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar (Special Olympics Zanzibar (SOZ).
Katika maongezi yao, Mheshimiwa Othman ameipongeza SOZ kwa mafanikio makubwa iliyoyapata na kuishauri juu ya haja ya kujiwekea mipango makini ikiwemo ya kujitangaza zaidi ili kuweza kutambulika kitaifa na kimataifa.
Aidha ametoa wito kwa Mamlaka zinazosimamia michezo Nchini, kuwekeza pia kwa Watu wenye Ulemavu wakiamini kuwa wanayo fursa kubwa ya kuitangaza Nchi na hatimaye kulijengea heshima Taifa katika medani ya Kimataifa.
Akieleza mafanikio ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa SOZ, Bi Sada Hamad Ali ametaja kiasi ya Medali 84 zikiwemo za Dhahabu, Fedha na Shaba ambazo Wachezaji wa Zanzibar wamefanikiwa kushinda kupitia Mashindano mbali mbali ya Olympics kwa Watu wenye Ulemavu wa Akili, Kitaifa na Kimataifa tangu kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1968.








0 comments:
Post a Comment