Nafasi Ya Matangazo

March 17, 2022

 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amemuelezea hayati Magufuli kuwa ni miongoni mwa  viongozi bora waliowahi kutokea Barani Afrika kwa namna alivyokuwa mtu mwema, mbunifu na mwenye moyo wa kulijenga taifa lake kwa upendo na kwa usawa.

Mhe. Spika ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yaliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita leo machi 17, 2022.

Aidha, Mhe. Dkt. Tulia amemshukuru na kumpongeza Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuyaendeleza mambo mazuri ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoanzishwa na hayati Magufuli kitendo alichokieleza kuwa ni kuwafuta machozi ya watanzania walio wengi.

 “Mheshimiwa Rais, siku ya leo ni siku ya kukumbuka mtangulizi wako alipoiaga dunia lakini tunafurahi kwamba kumbukizi hii haiji na majonzi tena bali inakuja na ushindi mkubwa ambao Mheshimiwa Rais umetufikisha hapa kwa kuyafanya mambo makubwa yakiwemo yale ambayo unayaendeleza kutoka kwa mtangulizi wako na zaidi yale ambayo unayafanya kwa utashi wako.” Amesisitiza Spika. Dkt. Tulia.

Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, yamehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali wa serikali, dini na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini.
Posted by MROKI On Thursday, March 17, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo