Nafasi Ya Matangazo

September 08, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akielekea leo katika ukaguzi wa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Usinge wilayani Usinge.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Matiko akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ambaye alikuwa na ziara ya utekelezaji wa wa agizo la Waziri Mkuu alilotaka uchunguzi wa matumizi ya fedha katika Kituo cha Afya cha Usinge.
***********
Na Lucas Raphael,Tabora
Hatimaye maangizo ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa yameanza kutekelezwa baada ya  kuundwa  kwa Kamati ya Uchunguzi   imepewa wiki moja  kutoa  taarifa sahihi  za  Matumizi ya shilingi Milion 600 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Usinge Wilayani Kaliua MkoaniTabora.

Kuundwa kwa kikosi kazi hicho ili kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wakati alipofanya ziara ya siku tatu mkoani Tabora  ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali .

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt.Batilda  jana wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo ili kutekeleza  agizo la  kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha katika Kituo cha Afya cha Usinge na mahali palipo hifadhiwa vifaa mbalimbali vya ujenzi huo.

Alisema kwamba  katika taarifa ya awali iliyotolewa na Mtendaji wa Kata ya Usinge kwa Kamati ya Usalama ya Mkoa iliyoonyesha uwepo wa akiba ya kiasi cha shilingi milioni 250 .

Aidha  alisema katika taarifa ya MKurugenzi Mtendaji kwa Waziri Mkuu ilionyesha kuwa wameshatumia kiasi cha zaidi milioni 600  na majengo bado hayajaisha.

Alisema baada ya taarifa hiyo kama kutakuwepo na ubadhirifu wa matumizi ya fedha katika mradi huo watakaobainika watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora Jerry Mwaga alisema katika taarifa waliyotoa kwa Waziri Mkuu hawakuweka gharama za vifaa ambavyo vilivyokuwa  katika ghala ambako walivihifadhi kwa ajili ya usalama.

Alisema kuwa hali hiyo ilifanya kuonekana kuwa fedha zilizotumika ni nyingi kuliko hali halisi kitu ambacho hakikuangaliwa mapema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Matiko alisema Kamati ya Uchunguzi inahusisha Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani, Wahandisi wa Wilaya wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira(RUWASA),Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) na Ofisi ya UsalamaWilaya(DSO)

Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika Kituo hicho hakuridhishwa na matumizi ya fedha na kazi ambayo imekwisha fanyika na kutoa miezi miwili kuhakikisha wamekamisha bila hata kuongeza fedha nje ya walizopatiwa.

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD), Wagonjwa wa Ndani(IPD) na Upasuaji na Jengo la Wazazi.

Posted by MROKI On Wednesday, September 08, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo