Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2021




Mkurugenzi wa Taasisi ya International Promotion Through Sports kutoka Brazil Bw. Paul Pan ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Malya mkoani Mwanza ili kuona ni jinsi tasisi hiyo itakavyoshirikiana na Serikali kukiboresha chuo hicho.

Bw.  Paul amefanya ziara hiyo Juni 24, 2021 kufuatia mazungumzo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa aliyofanya hivi karibuni na Balozi wa Brazil nchini Mhe. Antonio Augusto Cesar kukiboresha Chuo hicho kiweze kutoa taaluma ya michezo inayoendana na soko la ajira katika sekta ya michezo duniani ili chuo hicho kiweze kutoa elimu ya kuendeleza michezo nchini.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Yusuph Singo amesema ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na  Brazil utasaidia kuboresha chuo hicho ambachokitasaida kuibua na kukuza michezo nchini ambayo inatoa siko la ajira kwa vijana na wataalam wa michezo mbalimbali watakaoandaliwa na kuhitimu katika chuo hicho. 

Ziara hiyo Chuoni hapo ni matokeo ya kikao kilichofanyika Mei 21 2021 Jijini Dar es Salaam kilichofanywa na Mhe. Waziri Bashungwa na Balozi wa Brazil nchini ambacho ajenda yake ilikuwa kushirikiana katika sekta  maendeleo ya michezo nchini ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na programu ya kubadilishana wataalamu wa michezo kwa pande zote mbili za nchi hizo.

Posted by MROKI On Monday, June 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo