Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, Filemon Namwinga (kulia), akikabidhi Hatimiliki za Kimila kwa baadhi yawakulima wa zao la chai ambao mashamba yao yamerasimishwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya hiyo. Jumla ya mashamba 220 yamerasimishwa katika vijiji vitano vya Ilamba, Lusing'a, Magome, Kidabaga na Ng'ang'ange. Anayeshuhudia kulia kwake ni Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa MKURABITA, Anthony Temu.
Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Halmashauri hiyo, baada ya wanufaika hao kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kuzitumia hati hizo kuweka dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za fedha za kusaidia kuboresha miradi yao.
Mmoja wa wakulima akifurahia kupata hatimiliki za kimila.
Mmoja wa wakulima akitoa maelezo kuhusu maisha na mambo ya kiuchumi wakati wa kukusanya dodoso.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Emmanuel Mwakilema akitoa mafunzo kuhusu kanuni bora za kilimo cha zao la chai.Wakulima wakipatiwa hatimiliki zao.
Baadhi ya Wakulima kutoka vijiji vitano wilayani Kilolo wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
0 comments:
Post a Comment