Nafasi Ya Matangazo

January 15, 2025




WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 15, 2025 ameshiriki sherehe za uapisho wa Rais wa Msumbiji akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Maputo,  ambapo baada ya kiapo hicho  Rais Daniel Chapo ametaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa, kuimarisha usalama, kuboresha Sekta za elimu, afya na kilimo. 

Mbali na hayo Rais Chapo amewaomba wana Msumbiji wafanye kazi kwa ushirikiano pia ameahidi kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali kwa kupunguza  ukubwa wa Baraza la Mawaziri. 

Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane kutoka chama cha Podemos aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika  Oktoba 9, 2024. 

Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.

Viongozi wengine walioambatana na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uapisho huo ni Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Denis Londo na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdallah Hamid
Posted by MROKI On Wednesday, January 15, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo