Nafasi Ya Matangazo

February 04, 2020

Mfanyabiashara Faisal Shabhai ambaye anamiliki kampuni ya tanzaniteforever akizungumza.

Mwandishi wetu 
Arusha.Madalali 100 wa madini katika jiji la Arusha wamelipiwa leseni zao za kuendelea na kazi ya kuuza madini, kiasi sh 25 milioni.

Madalali  hao, wamelipiwa leseni hizo na mfanyabiashara wa madini, Faisal Shabhai na marafiki zake ambao sio Wafanyabiashara wa madini.
 Kamishna na Madini mkoa Arusha ,Hamis Kamando akizungumza katika mkutano na madalali hao alisema wamesaidiwa baada ya  kuamua kuwaomba Wafanyabiashara wakubwa wa Arusha

Alisema kuna madalali hawana uwezo na wapo wenye uwezo hivyo aliomba wadau  kuwasaidia kwa manufaa ya sekta ya madini

"Serikali ya awamu ya tano imekuwa ni ya kutetea wanyonge na Mimi kama Afisa Madini baada ya kubaini kuna madalali hawana uwezo wa kulipa leseni sh 250,000 niliamua kuomba wadau na  Faisal ndiye pekee alikubali"alisema

Alisema yeye binafsi anawalipia leseni madalalu wanne sh 1milioni kutoka katika mshahara wake.

Mfanyabiashara Faisal Shabhai ambaye anamiliki kampuni ya tanzaniteforever alisema yeye  na marafiki zake ambao si Wafanyabiashara wa madini kuwalipia lesseni madalali ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kusaidia wanyonge.

Alisema yeye kama mfanyabiashara  anaunga mkono jitihada za Serikali kuwasaidia wanyonge na anaamini kusaidia watu sio mpaka uwe na fedha nyingi.

Alisema anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kuhakikisha wanyonge pia wananufaika na rasilimali ya madini.

Alisema madalali ni watu muhimu katika sekta ya madini na wafanyabiashara wote wakubwa wamenufaika na uwepo wa madalali.

" Mimi na marafiki zangu leo tunarejesha shukrani hivyo mimi na rafiki zangu tutawalipia lesseni  madalali 100 ambao watapitishwa na chama chao na kuthibitishwa na Kamishna wa Madini mkoa.

Shabhai alimpongeza Rais Dk. John Magufuli,waziri wa madini na mkuu wa mkoa Arusha kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha watanzania wananufaika na madini.

Shabhai aliomba madalali wote kuruhusiwa kuingia Katika soko la madini hadi hapo mchakato wa leseni zao utakapokamilika maombi ambayo yalikubaliwa na Kamishna wa Madini.
Mwenyekiti wa chama cha madalali wa Madini mkoa Arusha,Jeremiah Simioni alimshukuru Faisal na Kamishna wa Madini mkoa Arusha Kwa kuamua kuwasaidia malalali Masikini.

Hata hivyo aliomba Serikali kupunguza Ada ya madalali kutoka 250,000 hadi 100,000 ili madadali zaidi ya 4000 wa mkoa Arusha wotewalipe leseni 

Madalali 520 pekee kati ya madalali zaidi ya 3000 ndio walikuwa wamelipia leseni zao.
Posted by MROKI On Tuesday, February 04, 2020 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo