CHAMA
CHA MAPINDUZI (CCM)
TAARIFA
KWA UMMA
KUHUSU
MCHAKATO WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA
VIJIJI MWAKA 2019
_______________
Ofisi ya Makao Makuu, Dodoma
10 Oktoba 2019
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wanachama wa CCM kuwa Mchakato
wa kuwapata wana CCM watakao simama katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
Vijiji unaendelea ndani ya Chama.
Ufuatao
ni mtiririko wa matukio ndani ya Chama ambao wanachama, viongozi na wanaoomba
kufikiriwa na kuteliwa na Chama wanapaswa kuuzingatia;-
NGAZI YA VIJIJI NA MITAA
Tarehe 7 – 12 Oktoba, 2019:
Kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kugombea Uenyekiti wa Mitaa, Vijiji na
Ujumbe wa Serikali za Vijiji na Mitaa kwa Makatibu wa Matawi ya CCM kote
nchini.
Tarehe 13 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Matawi kujadili wagombea na kutoa Mapendekezo yake kwa
Kamati za Siasa za Kata
Tarehe 14 – 15 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati
za Siasa za Wilaya
Tarehe 16 – 18 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kufanya uteuzi wa wagombea kwa
ajili ya kupigiwa kura za maoni na Mkutano wa Wanachama wote wa Tawi.
Tarehe 19 – 20 Oktoba, 2019:
Mikutano ya kura za Maoni ya nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa au Kijiji – Mkutano
wa Wanachama wote wa Tawi
BAADA YA KURA ZA MAONI
Tarehe 21 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Matawi kujadili wagombea na kutoa
mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu ya Kata
Tarehe 22 – 23 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Kata kujadili wagombea na kutoa
mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya
Tarehe 24 – 26 Oktoba, 2019:
Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Wilaya kujadili wagombea na kutuma
mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya.
Tarehe 27 – 28 Oktoba, 2019:
Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya Kufanya Uteuzi wa Mwisho wa Wanachama
watakaogombea Uenyekiti wa Mtaa, Ujumbe wa Kamati ya Mtaa, Uenyekiti wa Kijiji
na Ujumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
NYONGEZA: RATIBA YA SERIKALI
Tarehe 8 – 14 Oktoba, 2019:
Zoezi la uandikishaji wapiga kura siku saba tu kwa Mwananchi mkaazi wa Mtaa/
Kijiji na Kitongoji
Tarehe 29 Oktoba, 2019:
Kuanza kuchukua fomu za kugombea
Tarehe 4 Novemba, 2019:
Tarehe ya Mwisho ya kurejesha fomu kwa Msimamizi
Tarehe 10 Novemba, 2019:
Uwasilishaji wa ratiba za kampeni kwa Msimamizi
Tarehe 17 – 23 Novemba, 2019:
Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji
Tarehe 24 Novemba, 2019:
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji
Uongozi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli,
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unasisitiza wale
wote wenye sifa na wamekidhi vigezo na masharti ya uanachama wajitokeze
kuchukua fomu na kuomba kufikiriwa na hatimaye kuteuliwa. Fomu zinatolewa bure
katika Matawi ya CCM.
Tunatoa
rai kwamba Chama kinatarajia wana CCM wenye kuishi misingi ya Chama chetu watu
mahodari wa uadilifu, uaminifu, unyenyekevu, Wachapa kazi, wenye kazi
zinazowaletea kipato halali, watetezi wa kweli wa Maslahi ya wananchi,
wanaochukizwa na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma wajitokeze ili
wakakamilishe safu ya uongozi wa Serikali ya CCM inayotoa uongozi na kuleta
maendeleo makubwa kwa haraka katika nchi yetu chini ya Ndg. John Pombe Joseph
Magufuli.
Wanawake na vijana
wanahamasishwa kujitokeza kwa wingi kugombea.
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
HUMPHREY
POLEPOLE
KATIBU
WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
0 comments:
Post a Comment