Mbunge
wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo
akimkabidhi Afisa elimu Kata, Ruth Kisaka Mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata ya Msimbo wilayani Same, ikiwa ni
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Mbunge
wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk. Mathayo David Mathayo
akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mshewa, Anastazia
Clement kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020
Mbunge
wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo
akimkabidhi fedha taslimu diwani wa CCM kata ya Mhezi wilayani Same John Kiure
kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akihutubia wananchi.
MBUNGE wa Jimbo la Same
Magharibi CCM, Dk. Mathayo David Mathayo amewaomba wananchi
wa Jimbo la Same Magharibi kumuunga
mkono na kumuombea afya njema Rais John Magufuli ili aweze kuendelea kuiongoza
Tanzania izidi kupata maendeleo na kurudisha nidhamu katika sekta mbalimbali
nchini.
Dk.Mathayo ametoa kauli
hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza
wananchi wa jimbo hilo ambapo akizungumza na wananchi wa kata za Msindo,Mshewa
na Mhezi, Mathayo amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio lukuki
katika Nyanja mbalimbali.
Aidha Mbunge huyo
amekabidhi vifaa mbalimbali alivyoahidi katika kata hizo zikiwemo Fedha, saruji
na mabomba ya kusambazia maji huku akitoa rai kwa uongozi wa kila Kata
kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Katika Kata ya Msindo Dk.
Mathayo ametoa fedha ,mifuko ya saruji,mabomba ya maji,ambapo katika kata ya Mshiwa
amekabidhi mifuko ya saruji na fedha taslimu kwa ajili ya shughuli za
marendeleo kiasi cha shilingi milioni 13 laki 9 na Zaidi ya shilingi million
tisa katika kata ya Mhezi Zaidi ya shilingi milioni tisa na mifuko ya saruji.
0 comments:
Post a Comment