Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2019

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019, wa pili kutoka kushoto ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh na watatu kutoka kulia ni Mke wa Balozi Doanh pamoja na maafasia ubalozi huo wakishuhudia tukio hilo. 

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi kupitia kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini nakuelezea kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.
Profesa Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi Doanh
************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019.

Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi huo wa Vietnam Profesa Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi wa Vietnam na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.

Ameongeza kuwa Uhusiano baina ya Jamhuri ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa umekuwa katika nyanja ya kiuchumi hususani katika eneo la mawasiliano ambapo ameitaja kampuni Halo tell kama mojawapo ya kampuni iliyowekeza katika sekta ya mawasiliano.

Ameyataja mahusiano mengine yapo katika sekta ya kilimo hususani katika kilimo cha korosho na kahawa na kwasababu hizo kama mataifa Rafiki ya muda mrefu amefika katika ubalozi huo kwa ajili ya kuhani msiba wa aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 98.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya watu wa Vietnam hapa nchini Balozi Nguyen Kim Doanh,amshukuru Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Amemtaja Jenerali Le Duc Anh kama mmoja wa viongozi waliokuza kwa kiasi kikubwa mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kwamba ana matumaini makubwa kwa siku za usoni mahusiano baina ya nchi hizi mbili yataendelea kukuzwa na kuimarishwa.
Posted by MROKI On Saturday, May 04, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo