Nafasi Ya Matangazo

May 27, 2019


Mkurugenzi wa UNILIFE CAMPAS, Dosi Said Dosi wakati akitoa somo la kujitambua kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ajili ya kuwajengea uwezo wa kujiwekea akiba yaliyoandaliwa na UNILIFE CAMPAS jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakifuatilia.
 Meneja wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Alphonce Musiba akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa fedha mapema leo wakati wakitoa masomo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kujiwekea akiba yaliyoandaliwa na UNILIFE CAMPAS jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Smart Me App, Innocent Mathias amewataka vijana wenzake kuwa msitari wa mbele kuweka malengo yao katika masomo huku wakijiwekea akiba katika kipato cha fedha wanazopata.
Mwanzilishi mwenza wa Smart Me App, Edger Lwambano nnocent akiongea machache.

Afisa Mauzo wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili, Jane Haule akitoa machache kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
 Wanafunzi wakipata maelezo mbali mbali juu ya kufungua akaunti.
 Kila mmoja busy na kazi...
 Afisa Mauzo wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Jane Haule akiwafungulia akaunti ya malengo wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
 Majadiliano kidogo yakiendelea.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason - Kajunason/MMG.
Wanafunzi wa vyuo wametakiwa kuweka malengo katika matumizi yao ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Unilife Campas, Dosi Said Dosi wakati akitoa somo la kujitambua kwa wanachuo wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.

Dosi amesema kuwa ipo haja ya wanafunzi kuanza kujiwekea akiba ya fedha na kujihusisha na miradi midogo midogo itakayoweza kuwavusha hata pindi watakapomaliza chuo.

"Wakati umefika kila mmoja wetu kujiwekea akiba ya kile kidogo ambacho unakipata sasa maana huko mbeleni ukimaliza chuo utakuta umeweka kidogo kuliko kumaliza akiba yote," amesema Dosi.

Ameongeza pia kuwakaribisha vijana wanachuo na waliomaliza kufika ofisi za Unilife Campus kuweza kuwapatia elimu ya namna ya kuanzisha kampuni za aina mbalimbali bure ili waweze kujiajiri.

Kwa upande wake wa Meneja wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Alphonce Musiba amewaomba vijana kuendelea kuwa wabunifu wa kubuni miradi huku wakijiwekea akiba kwa pesa kidogo wanazozipata.

"Ukiwa chuo unakuwa na nafasi nyingi za kupata fedha hasa kwa wazazi, walezi na wengineo sasa ni vyema kuwa na adabu nazo ili zikuvushe katika maisha yako," amesema .

Ameongeza kuwa kwa sasa benki ya NBC wameanzisha akaunti ya kuwawezesha wanafunzi kujiwekea akiba kidogo kidogo ili waweze kufikia malengo yao.

Nae mwanzilishi wa Smart Me App, Innocent Mathias amewataka vijana wenzake kuwa msitari wa mbele kuweka malengo yao katika masomo huku wakijiwekea akiba katika kipato cha fedha wanazopata.

"Binafsi nimefanikiwa kujiwekea akiba mpaka leo nimefika hapa nilipo kwa ajili ya adabu na heshima katika matumizi ya fedha ninazopata nikiwa chuo, tuweke akiba hata ikiwa shilingi 500 baadae unakuwa na kiasi kikubwa tu. Hivyo nawaasa wanafunzi wafungue akaunti ya kuhifadhi fedha pamoja kupitia SmartMe ili ziweze kuwanufaisha baadae.
Posted by MROKI On Monday, May 27, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo