Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhe. Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.

Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Mhe. Peter Eriksson.

Baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Peter Eriksson amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake kwa mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya rushwa na ameeleza dhamira ya Sweden kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia picha ya kuchorwa Mhe. Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden alipokutana na kufanya
naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Andres Sjoberg.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kaatika picha ya pamoja na  Mhe. Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden na ujumbe wake pamoja na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Andres Sjoberg.
Posted by MROKI On Monday, May 20, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo