Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi nyenzo za kazi Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.

Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Dkt. Mpoki Mwasumbi Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada.

Hafla ya kuapishwa kwa Mhe. Balozi Ulisubisya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Posted by MROKI On Monday, May 20, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo