Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akimkabidhi mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle cheti cha ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Kulia ni Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania. Grace Mgaya. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mkuu wa shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau akifurahi baada ya kupokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana mara baada ya shule hiyo kufanikiwa kutoa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg
Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akikabidhiwa kikombe cha ushindi na Mkuu wa shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akifurahi na wazazi wake Calvin Marealle na Jamila Marealle mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (Kulia) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto) wakikabidhi seti ya DStv kwa mkuu wa shule ya sekondari St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau na mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg wakati shule yake imepata cheti na zawadi ya kufungiwa huduma ya DStv.
***********
Kwa mara nyingine tena Tanzania imeibuka kinara katika tuzo za kimataifa za wanafunzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards ambapo mwanafunzi Priscilla Marealle kutoka shule ya sekondari ya St. Mary Goreti mkoani Kilimanjaro ameweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa kunyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha uchoraji bango ikiwa ni baada ya mchuano mkali baina ya mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika.
Kwa upande wa uandishi wa insha kijana Tanaka Chonyera kutoka nchini Botswana aliweza kujinyakulia ushindi wa kwanza.
Tuzo hizi ambazo huhusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango yenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.
Katika msimu huu wa nane, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango litakaloelezea licha ya Satelait kutumika katika shughuli mbalimbali, ni namna gani zitaweza kutumika zaidi ili kuleta maendeleo chanya ulimwenguni.
Priscilla ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita wa mchepuo wa Sayansi katika shule ya Mtakatifu Maria Goreti alitangazwa rasmi kuwa mshindi mjini Accra nchini Ghana ambapo ndipo jopo la watahini liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European Space Agency (ESA) lilikaa kupitia kazi kutoka kwa wanafunzi walioshinda katika nchi mbalimbali.
Akiongea baada ya kukabidhiwa cheti cha uthibitisho wa ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule ya Mtakatifu Mary Goreti iliyopo Moshi Kilimanjaro, Priscilla amesema amefurahi sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri. Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi, na kusisitiza kuwa Ndoto huanza kufanya kazi pale unapojiamini” alisema Priscilla.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mtakatifu Maria Goreti Sister Lucresia Njau alisema kuwa anaishukuru sana kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika Mashindano hayo na hatimaye kuweza kunyakua tuzo hiyo kupitia mwanafunzi wao Priscilla.
“Huyu kijana ana jitahidi sana katika chochote kile anachokifanya, iwe ni darasani au hata katika majukumu mengine nje ya darasani. Ni msikivu mtiifu lakini zaidi ya yote ni mbunifu sana. Naamini haya ndiyo yaliyomfanya aweze kushinda tuzo hizi” alisema Sr. Lucrecia Njau.
Naye, Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alisema,” Huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa Tanzania kuendelea kung’ara katika tuzo hizi za DStv Star Awards. Tulianza kupeperusha bendera yetu na kijana Davids Bwana msimu wa sita baada ya kushika nafasi ya pili Afrika katika kipengele cha uandishi wa insha, kisha tukaibuka kidedea baada ya kupokea taarifa za ushindi wa kwanza wa kijana Taheer Rashid katika msimu wa saba mwaka jana na leo hii tunayofuraha kubwa kuona kuwa tumeendeleza wimbi la ushindi.”
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Pricilla kutangazwa kuwa mshindi, walimu na wazazi wa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita mwenye umri wa miaka 19, wamesema kuwa wanamfahamu vyoma Pricilla kuwa ni kijana mwenye kupenda kujibidisha sana katika masuala ya kitaaluma na kijamii hivyo ushindi wake ni kitu kilichotarajiwa na kwamba wanaamini kuwa anastahili ushindi huo.
Pamoja na kupata cheti maalum cha ushindi, Pricilla atapata fursa (Yeye na Mzazi au mlezi) ya kutembelea kitua cha Anga cha Afrika Kusini na pia kutembelea makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg kama mgeni maalum wa DStv huku shule aliyotoka ikipata zawadi ya cheti pamoja na kufungiwa huduma ya DStv.
0 comments:
Post a Comment