KATIKA kusherehekea sikukuu ya wanawake Duniani Machi 8, Leo akina mama na Vijana wilayani Busega wamepatiwa vyerehani,mashine za kufyatulia matofali na mashine za kusaga nafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Raphael Chegeni kwa kuwawezesha wanawake na vijana kwani kupitia vifaa hivyo wanaweza kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono kwa vitendo Falsafa ya Rais John Magufuli ya HAPA KAZI TU.
Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa wanawake na vijana.
Vitu mbalimbali ambavyo Mbunge wa Busega amevigawa kwa wanawake na Vijana leo.
Mbunge wa Busega na Viongozi wengine mbalimbali wa Wilaya wakiwa meza kuu.
0 comments:
Post a Comment