Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha United Sports Club Otte Beda Ndaweka
TIMU ya Arusha United Sports Club, inayoshiriki
ligi daraja la kwanza imetangaza kujitoa rasmi katika ligi hiyo kwa
madai ya kuchoshwa na vitendo ambavyo si vya kimichezo huku TFF
kupitia bodi ya ligi ikishindwa kuchukua hatua stahiki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo Otte Beda Ndaweka amesema kuwa licha
ya timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri katika kundi B imeona si buasara
kuendelea na ligi hiyo kufuatia matukio mbalimbali ikiwemo kufanyiwa vurugu
wakati ikicheza na timu kadhaa tangu timu hiyo ianze kushiriki ligi hiyo msimu
wa mwaka 2018-2019.
Aidha Ndaweka amesema licha ya timu hiyo kuwa
na vibali vya kurekodi michezo yake yote ya ligi kuanzia mchezo wake dhidi ya
Dodoma Fc uliofanyika mjini Dodoma bodi hiyo pia imeshindwa kuhakikisha
maelekezo,miongozo au vibali vyake vinaheshimiwa na au kuchukua hatua pale
ambapo haviheshimiwi.
Timu ya Arusha United ni moja ya timu
zinazoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa kundi B,kwa sasa ikiwa
imekwisha cheza michezo 17 kukusanya jumla ya point 28 huku ikishika nafasi ya
tano ambapo timu ya Geita gold FC ikiongoza ligi hiyo ikiwa na point 33.
0 comments:
Post a Comment