Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2019

Mwandishi wetu,Arusha, 
Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori nchini(TAWA) imewataka   wamiliki wa vitalu vya uwindaji nchini, kufuata sheria na kanuni za umiliki wa vitalu  la sivyo watanyang'anywa vitalu hivyo.

Mkurugenzi mkuu wa TAWA, Dk James Wakibara alitoa   jijini Arusha, wakati akizungumza na  juu ya matukio ya ujangili nchini na jitihada za kumaliza matukio ya ujangili ambazo zinafanywa na serikali na wadau wa utalii.

Dk Wakibara alisema ni lazima wamiliki wa vitalu, kuhakikisha wanazuia ujangili katika vitalu vyao na maeneo ya jirani, lazima pia wawe na mahusiano mema na jamii zinazowazunguka.

Hata hivyo alisema,  baada ya kudhibitiwa ujangili wa Tembo katika maeneo mengi nchini, umeibuka ujangili wa nyama katika baadhi ya maeneo hasa katika maeneo ya mapori tengefu.

Hata hivyo, alisema kumeanza kuripotiwa baadhi ya matukio ya ujangili hasa wa nyama, katika maeneo ya mapori tengefu ambayo baadhi ni vitalu vya uwindaji.

Alisema kama ikibainika mmiliki wa kitalu, anashindwa kuwa na ulinzi na anashindwa kufuata sheria na taratibu, waziri wa Maliasili na Utalii, anaweza kumuondoa.

Naibu Mkurugenzi wa TAWA masuala ya uhifadhi na kuzuiwa ujangili,, Mabula Misungwi  alisema matukio ya ujangili yamepungua katika maeneo mengi nchini na sasa kumeibuka ujangili wa wanyama kwa ajili ya chakula na mahitajji mengine ambao lazima udhibitiwe.

Hivi karibuni, imebainika wilaya ya Longido, kuibuka ujangili wa Twiga ambapo Twiga 25 waliuawa na majangili ndani ya miaka miwili na tayari watuhumiwa watano wanashikiliwa na jeshi la polisi huku wengine 20 wakidaiwa kukimbilia nchi jirani.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pia ameunda kamati nyingine ya kitaalam kuwahoji watuhumiwa wote waliobainika katika tume ya awali ili kujua mtandao mzima wa mauaji ya Twiga.
Posted by MROKI On Tuesday, February 19, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo