Nafasi Ya Matangazo

January 04, 2019

Kampuni ya MultiChoice Tanzania, imekabidhi jingo la nyumba mbili za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja Zanzibar katika hafla iliyofanyika shuleni hapo hivi karibuni na kuongozwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso.


Jengo la nyumba za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja lililojengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.

Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa za walimu ulifanywa na wananchi wa Kizimkazi na kufadhiliwa na MultiChoice Tanzania ambayo ilichangia takriban shilingi milioni 120 katika kukamilisha mradi huo.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (wa pili Kulia. Mku wa Mkoa wa Kusini Unguja Hassan Khatib Hassan. (Kulia), Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Madinnah na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso (Kushoto) wakiwasili katika shule ya Kizimkazi tayari kufungua rasmi jengo la nyumba za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo lenye nyumba mbili za walimu limejengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa nyumba hizo, Waziri Kombo ameelezwa kurudhishwa kwake na kiwango cha ujenzi wa nyumba hizo na kubainisha kuwa mradi huo umekamilika kwa haraka na kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na mchango mkubwa wa MultiChoice Tanzania.

Amesema nyumba hizo zitakuwa mkombozi mkubwa kwa walimu ambao walikuwa wakitaabika kwa usafiri kutokana na kuishi mbali na shule, suala ambalo lilichangina sana katika kupunguza ufanisi wa kazi. “Kwa nyumba hizi, sasa tuna uhakika wa waalimu wengi zaidi kuishi karibu na maeneo ya shule hivyo kuwa na muda wa kutosha kuwa karibu na wanafuzi na hili bila shaka litachangia sana kuboresha elimu hapa Kizimkazi” alisema Waziri Kombo.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso (Kushoto) wakikata utepe kufungua rasmi jengo la nyumba za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo lenye nyumba mbili za walimu limejengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema mradi huo ni muendelezo wa uwekezaji mkubwa wa MultiChoice katika miradi ya kijamaa kote nchini. “MultiChoice imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwamo elimu, na ufadhili huu ni ishara tosha ya ushiriki wetu katika kuleta maendeleo ya jamii yetu”.


“Miezi michache iliyopita tulikubali wito wa Muheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (Ambaye ni mwenyeji wa wapa Kizimkazi) wa kuiomba MultiChoice kusaidia katika kukamilisha jingo hili la nyumba za walimu nasi kwa kutambua umuhimu wa elimu na kwakuwa sisi Multichoice tunaamini katika uwekezaji kwenye sekta za kijamii, basi tulikubali ombi lake na kuridhia kukamilisha ujenzi huo kwa gharama ya takriban shilingi milioni 120 ili kuwawezesha walimu wetu kuwepo karibu na wanafunzi na hivyo kuweza kufuatilia maendeleo yao kwa karibu zaidi” alisema Jacqueline.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (wa tatu kulia - waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso (wa pili kulia) na maafisa mbalimbali waandamizi wa Zanzibar muda mfupi baada ya kufungua rasmi jengo la nyumba za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo lenye nyumba mbili za walimu limejengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.

Pia Mkurugenzi huyo aliridhia ombi la Waziri Komba kuiomba MultiChoice Kuchangia katika kuseka samani katika nyumba hizo. Pia MultiChoice ilitoa seti za ving’amuzi vya DStv kwa ajili ya kufungwa katika nyumba hizo ili kuwawezesha walimu kupata habari burudani na elimu mbalimbali kupitia DStv na hivyo kupanua zaidi ufahamu wao na hatimaye kuwa walimu bora zaidi .
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akipokea seti ya DStv kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso kwa ajili ya kufungwa kwenye nyumba mpya za walimu wa shule ya Kizimkazi Kusini Unguja. MultiChoice Tanzania imefadhili ukamilishaji wa jengo lenye nyumba mbili za walimu ambapo imechangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.
Posted by MROKI On Friday, January 04, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo