Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2019

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wa pili kutoka kushoto, Bi. Veronica Hellar, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Prof. Lawrence Museru akimshukuru muwakilishi kutoka The German Society for Tropical Paediatrics (GTP), Dkt. Antke Zuechner (wa pili kutoka kulia) kwa kutoa msaada wa mashine ya Utrasound ambayo itatumika katika wodi ya watoto wachanga kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya moyo, kichwa na tumbo.
Dkt. Zuechner akiwapatia maelezo watalaam wa Muhimbili namna ya kutumia mashine hiyo ambayo imetolewa kwa ajili ya wodi ya watoto wachanga.
Dtk. Zuechner akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Muhimbili mara baada ya kukabidhi mashine hiyo.



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepatiwa msaada wa mashine ya kisasa ya Utrasound ambayo itatumika katika wodi ya watoto wachanga kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya moyo, kichwa na tumbo. 

Mashine hiyo yenye teknolojia ya juu na uwezo mkubwa wa kuchunguza magonjwa hayo ina thamani ya dola za kimarekani 17,000 imetolewa na Taasisi ya Kijerumaini inayoitwa The German Society for Tropical Paediatrics (GTP). 

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, Mkuu wa Kitendo cha Sheria katika hospitali hiyo Bi. Veronica Hellar amesema mashine hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuwahudumia watoto wachanga hivyo itatumika kama ilivyokusudiwa. 

“Tunashukuru kwa msaada huu mliotupatia ambao umekuja wakati muafaka hasa ukizingatia lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto,” amesema Bi. Hellar. 

Kwa upande wake muwakilishi kutoka taasisi hiyo Dkt. Antke Zuechner amesema msaada huo una lenga kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Muhimbili katika kuhudumia watoto wachanga. 

Watalaam wa MNH watapatiwa mafunzo maalum ili kuweza kutumia mashine hiyo ambayo ni ya kisasa zaidi.
Posted by MROKI On Friday, January 11, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo