Nafasi Ya Matangazo

January 14, 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan, Mhe. Shinichi Goto aliyeambatana na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda Nchini Japan kwa ajili ya kupata mafunzo ya Uongozi katika sekta mbalimbali. Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa siku 50. Aidha, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Goto kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi ya Japan hapa nchini ambapo aliahidi kuwa Japan itaendelea kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali. 

Dkt. Ndumbaro amewaasa Washiriki wanaokwenda katika mafunzo hayo kuitumia fursa hiyo vyema kwa kujifunza mambo mampya kutoka Taifa hilo. 

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Caesar Waitara (hayupo pichani) yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar Es Salaam.
Mazungumzo yakiendelea 
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Goto
Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi Goto wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda nchini Japani. 
Posted by MROKI On Monday, January 14, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo